Main Title

source : ParsToday
Jumatatu

6 Januari 2020

06:33:51
999751

Sheikh Naim Qassem ahani msiba nyumbani kwa Kamanda Soleimani; asema mapambano yataendelea kwa nguvu zaidi

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesema kuwa ni wazi kuwa njia na mstari wa mapambano utaendelea kwa nguvu zaidi kufuatia kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na wenzake aliokuwa amefuatana nao.

(ABNA24.com) Sheikh Naim Qassem Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon leo Jumapili amekwenda kuhani msiba nyumbani kwa shahidi Luteni Jenerali Soleimani hapa Tehran na kubainisha mbele ya waandishi wa habari kwamba: Marekani imetenda ushenzi mkubwa kwa kitendo chake hicho cha kigaidi.

Sheikh Naim Qassem amesema kuwa njia ya muqawama itaendelezwa kwa nguvu zote na hakuna shaka kwamba njia hiyo itaimarishwa zaidi baada ya kuuliwa shahidi Kamanda Soleimani.  

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa mapambano yataendelea hadi kuangamizwa kikamilifu Israel. Amesema mapambano yataendelezwa ili kufelisha malengo ya Marekani katika eneo.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds katika jeshi la Sepah na Abu Mahdi al Muhandes Naibu Mkuu wa kikosi cha al Hashd al Shaabi cha Iraq pamoja na watu wengine wanane waliokuwa nao waliuawa shahidi Ijumaa alfajiri iliyopita katika shambulio la anga la wanajeshi vamizi wa na magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad mji mkuu wa Iraq.  

Wakati huo huo Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Jawad Shaharistani Mwakilishi wa Ayatollah Sistani marja mkuu nchini Iraq leo Jumapili pia amekwenda kuhani msiba nyumbani kwa shahidi Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Sepah.

Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Jawad Shaharistani Mwakilishi wa Ayatollah Sistani ametoa mkono wa pole na taazia kwa familia ya Kamanda Soleimani kufuatia kuuliwa shahidi Kamanda  huyo wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH).

...........
340