Main Title

source : ParsToday
Jumatatu

6 Januari 2020

06:33:56
999753

Kiongozi wa Russia: Jenerali Qassem Soleimani alikuwa shujaa wa ulimwengu wote wa Kiislamu

Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa inayoitwa 'Umma Mmoja wa Kiislamu' nchini Russia amesema kuwa, Meja Jenerali Qassem Soleimani, hakuwa tu mtu wa Iran, Iraq au Syria, bali ni shakhsia wa Kiislamu na ulimwengu kwa ujumla.

(ABNA24.com) Mohammad Amin Majumder ambaye miaka kadhaa iliyopita alikuwa mkuu wa Federesheni ya Wahajiri huko Russia ameyasema hayo katika mahojiano na Shirika la Habari la IRNA na kuongeza kuwa Jenerali Soleimani alikuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya magaidi wa genge la Daesh (ISIS) na pia katika kukabiliana na njama chafu za ubeberu wa dunia na Uzayuni unaoongozwa na Marekani.

Kiongozi huyo wa Russia ameendelea kubainisha kuwa, Jenerali Qassem Soleimani, alikuwa jenerali wa mioyo ya watu ambaye nchi nyingi za Kiislamu zilikuwa zinamkubali mwanamapambano huyo aliyekuwa akipigana katika njia ya Mwenyezi Mungu na kwamba shakhsia kama huyo hatosahaulika.

Mohammad Amin Majumder amesisitiza kuwa, shahidi Luteni Jenerali Soleimani kamwe hakuzingatia maslahi yake binafsi kama ambavyo hakufuatilia faida katika kukabiliana na njama za maadui wa Uislamu na katika njia hiyo alivumilia shida na matatizo mengi.

Aidha amesema kuwa hii leo maulama wa Kiislamu wana wadhifa mzito na ni lazima wasimame imara kukabiliana na njama za kuibua mifarakano za maadui wa Uislamu na dhidi ya umoja wa Waislamu.

Mohammad Amin Majumder ameongeza kuwa, njia aliyoifuata shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani ndio njia ile ile ya Mtume Muhammad (saw) ambayo iliwekewa misingi na Mwasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam Khomeini (MA) na Kiongozi Muadhamu Sayyid Ali Khamenei.

.........
340