Main Title

source : ParsToday
Jumatatu

6 Januari 2020

06:33:56
999754

Waziri wa Ulinzi wa Iran; Ulimwengu mzima una wajibu wa kukabiliana na hatua ya kigaidi ya Marekani

Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema kuwa ulimwengu mzima una wajibu wa kukabiliana na hatua ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Kamanda Qassem Soleimani; na watu wote wanapaswa kutekeleza majukumu yao mbele ya jinai hiyo.

(ABNA24.com) Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na Abu Mahdi al Muhandes Naibu Mkuu wa kikosi cha wapiganaji wa kujitolea wa Iraq (al Hashd al Shaabi) pamoja na watu wengine wanne waliokuwa nao waliuliwa shahidi Ijumaa alfajiri katika shambulio la anga la wanajeshi vamizi na magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.

Brigedia Jenerali Amir Hatami Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema leo hapa Tehran katika shughuli ya kumbukumbu ya mwaka wa 25 tangu kufa shahidi Meja Jenerali Mansour Satari kamanda wa zamani wa kikosi cha anga cha jeshi la Iran na kuongeza kuwa: Kitendo cha kuamuru kuuliwa kamanda wa ngazi ya juu akiwa katika ziara rasmi ya kuitembelea nchi nchi jirani akiwa na mwenyeji wake ni kinyume na sheria za kimataifa; na jinai kama hii haijawahi kushuhudiwa katika historia.   

Brigedia Jenerali Amir Hatami ameongeza kuwa Marekani imetoa amri ya kutekelezwa mauaji hayo kutokana na kukata tamaa kwake pakubwa; na inabeba dhima ya jinai hiyo. Amir Hatami amesema Marekani imesajili jina lake katika historia kwa kutenda jinai hiyo ya kivita.

Brigedia Jenerali Amir Hatami ameashiria pia mapambano ya shahidi Luteni Jenerali Soleimani katika mhimili wa muqawama na kuliangamiza kundi la Daesh na kueleza kuwa: Kundi hilo halikutarajiwa kuangamizwa kwa sababu Wamarekani ndio walioliasisi na kutaka kundi hilo liendelee kuwepo hata hivyo vikosi vya wanamuqawama vimefelisha kabisa njama za uistikbari wa dunia. 

..........
340