Main Title

source : ParsToday
Jumatatu

6 Januari 2020

06:44:56
999767

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amejibu tishio alilotoa Ras wa Marekani dhidi ya wananchi wa Iran kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusisitiza kuwa: Tishio hilo dhidi ya maeneo ya kiutamaduni ni jinai ya kivita.

(ABNA24.com) Rais Donald Trump wa Marekani amesisitiza katika radiamali yake hiyo kuhusu kulipiza kisasi Iran kwa hatua ya kigaidi ya Marekani ya kumuua Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na kudai katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: Marekani itashambulia maeneo 52 nchini Iran katika kuwawakilisha raia 52 wa Marekani waliotiwa mbaroni miaka kadhaa iliyopita wakati wa kushambuliwa ubalozi wake iwapo Iran itamshambulia raia yoyote wa Marekani au maslahi ya nchi hiyo.

Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliandika jana katika ukurasa wake wa Twitter kuwa Rais Donald Trump wa Marekani amekiuka wazi sheria za kimataifa kwa mauaji hayo ya kigaidi na ya uoga ya karibuni; na kwa mara nyingine tena ametishia kukiuka upya kanuni za kimataifa.

Zarif amesisitiza kuwa kitendo cha kuyalenga maeneo ya kitamaduni ya Iran ni jinai ya kivita na kuongeza kuwa mwisho wa kuwepo kwa ushari wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi umeanza.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods katika jeshi la SEPAH na Abu Mahdi al Muhandes Naibu Mkuu wa Harakati ya al Hashd al Shaabi ya Iraq na watu wengine wanane waliuawa shahidi Ijumaa iliyopita alfajiri katika shambulio la anga la kigaidi la  Marekani  karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, Iraq.

...........
340