Main Title

source : ParsToday
Jumatatu

6 Januari 2020

06:44:56
999768

Nasrullah: Siku ya kuuawa shahidi Kamanda Soleimani, mwanzo wa historia mpya Mashariki ya Kati

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tarehe 3 Januari 2020 ambayo ni siku ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, ni mwanzo wa historia mpya katika eneo la Mashariki ya Kati.

(ABNA24.com) Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, Sayyid Hassan Nasrullah amesema hayo jioni ya leo katika kumbukumbu maalumu ya kuuawa shahidi Kamanda Brigedia Jenerali Qassem Soleimani pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la Hashd al Shaabi waliouliwa kigaidi kwa roketi lililorushwa na helikopta ya Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad Iraq, usiku wa kuamkia Ijumaa ya tarehe 3 Januari, 2020. Kumbukumbu hizo zimefanyika katika eneo la kusini mwa Beirut leo Jumapili.

Katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Soleimani akiwa pamoja na al Muhandis kumefanyika kwa amri ya moja kwa moja ya rais wa Marekani, Donald Trump ambaye naye amekiri kufanya jinai hiyo.

Amesema, ushindi wa kambi ya muqawama katika nchi za Syria, Lebanon, Palestina, Iraq, Yemen na pia suala la kukaribia uchaguzi nchini Marekani ni miongoni mwa sababu zilizoifanya Marekani itangaze hadharani kuhusika katika mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Sayyid Nasrullah aidha amesema, kushindwa njama zote za Trump mbele ya Iran ni sababu nyingine muhimu ya kuuliwa kigaidi Kamanda Soleimani na kuongeza kuwa, lengo la Trump ni kuipindua Jamhuri ya Kiislamu ya Iran au kwa uchache kuipigisha magoti na kuilazimisha ikubali kuburuzwa na Marekani lakini ameshindwa kufikia lengo lake hilo. Vile vile amesema, hata kiatu cha Luteni Jenerali Soleimani kina thamani zaidi kuliko kichwa cha Donald Trump.

..........
340