UN: Wavulana milioni 115 duniani wako katika ndoa za utotoni
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umesema katika kila watoto watano duniani, mmoja yuko katika ndoa za utotoni, huku watoto wa kiume zaidi ya milioni 115 kote duniani wakijikuta katika ndoa hizo wakiwa na chini ya umri wa miaka 15.