Main Title

source : abna.ir
Jumanne

28 Oktoba 2014

19:47:29
647547

Katika harakati zote za kidini tangu enzi za manabii, mpaka hivi sasa, kumewepo na wapinzani wa dini, wapinzani wa dini wamekuwa na hoja mbali mbali katika upinzani huo. Wapinzani wa dini tunaweza kuwagawanya katika makundi mawili. Wapinzani wa dini wa zamani (enzi za manabii) na wapinza wa dini wa sasa

Hoja za wapinzani wa dini:
Katika harakati zote za kidini tangu enzi za manabii, mpaka hivi sasa, kumewepo na wapinzani wa dini, wapinzani wa dini wamekuwa na hoja mbali mbali katika upinzani huo.
Wapinzani wa dini tunaweza kuwagawanya katika makundi mawili.
Wapinzani wa dini wa zamani (enzi za manabii) na wapinza wa dini wa sasa.
Wapinzani wa dini wazamani waliwapinga manabii kwa kusema kwamba wao si malaika hivyo hawana mamlaka ya kujikwenza na kujifanya wanamahusiano na Mungu, pia waliitwa wachawi, hasa baada ya kuonyesha mambo ambayo yako nje ya uwezo wa mwanadamu wa kawaida.

Wapinzani wa sasa (makomonist)wamekuja na hoja na fikra zifuatazo katika kupinga kwao dini:
(i) Dini inapinga sayansi na elimu za kisasa.
(ii) Dini ni dawa iliyogunduliwa na mabepari ili kuwatuliza watu wa tabaka la chini, na kuwafanya watosheke na hali yao hiyo ya kimaskini,kwa ibara nyingine dini ni mchezo wa kisiasa wa kuwafanya watu wasifikirie dhulma wanazofanyiwa, kwani dini inawahimiza kuwa wavumilivu.

Basi hebu ngoja tutafakari kunako hoja hizi ili tupate tafakuri na ukweli kuhusu hoja hizi ambazo zimekuwa zikizungumziwa na wanazuoni wengi tangu Karl Marx hadi Bertrand Russell) hawa walikuwa ni wakristo na walikosea kuhukumu kwa mtazamo wa dini moja tu, kwani duniani kuna dini nyingi kama Uyahudi, uislamu na n.k.
Hoja ya kwanza ya kuingana dini na sayansi haikusanyi dini zote bali ni kupingana dini ya kikristo na sayansi.
Ili kuueleza kinagaubaga usemi huo hapo juu, inatulazimu kueleza kwa muhtasari tu hali ilivyokuwa kati ya ukristo na sayansi.
Tangu karne ya kumi na sita ya baada ya Yesu kristo,kulitokea upinzani na malumbano kati ya Kanisa na sayansi. Upinzani huu haukuanzishwa na wanasayansi, bali ulianzishwa na viongozi wa kanisa; ambao walihofu kuwa dini yao ilikuwa katika hatari kubwa ya kupoteza nguvu zake miongoni katika waumini wa kikristo. Ngome ya mafundisho yao ilikuwa katika hatari ya kuanguka. Madhehebu yote mawili ya kikristo (Katoliki na Protestanti) ingawa madhehebu haya yalikuwa na marumbano yenyewe kwa yenyewe, madhehebu haya yalikuwa na msimamo mmoja kuhusu upinzani uliyopo baina ya mafundisho ya kikristo na njia za kimapinduzi za kisayansi, za Bwana Cupernicus, na mwenzie bwana Galileo.
Kanisa liliwaadhibu wanasansi hawa kwa kuwa walikuja na mitazamo ya kielimu inayopingana na mitazamo ya kanisa,
(1) "Tukianza na Bwana Cupernicus (Nicolaus Koppernigh) aliyeishi kati ya mwaka 1473-1545, maana yeye ndiye aliyeanzisha fikra pinzani, Bwana huyu kwa kuwa alikuwa akiogopa uongozi wa kanisa alikaa kimya kwa muda mrefu na hakuthubutu hata kuchapisha kitabu chake, chenye upinzani huo, kijulikanacho kwa jina la "On the Revolution of Heavenly Bodies" (katika mzunguko wa sayari za Angani)."
Mwishoni alifaulu kulituliza Kanisa kwa kukiandika kitabu hicho kwa heshima ya Papa.Mchapishaji wa kitabu hiki aliandika utangulizi kuthibitisha kuwa maelezo juu ya mzunguko wa dunia ni jambo linalokubaliwa tu, wala si jambo Iililothibitishwa kabisa.
Muhatasari ni kwamba kanisa lilikuwa likipinga kuwa dunia inazunguka, nakwamba dunia ni duara, wanasayansi walithibitisha kuwa dunia ni duara na inazunguka. Baada ya kuthibiti kuwa dunia ni duara na inazunguka heshima ya kanisa ilishuka na kuonekana kuwa kanisa linafundisha mafunzo yanayokinzana na elimu ya sayansi.

(2) Mwanasayansi mwingine, Bwana Galileo Galilei aliyeishi kati ya mwaka 1564-1642 Masihiy, ingawa alikuwa rafiki wa Papa Urban VllI, alitiwa katika jela kwa kosa la kuzusha mambo katika dini, kwa amri ya Papa huyo na kutishiwa atapata mateso makali kama hataacha mafundisho yake yanayokinzana na mafunzo ya kanisa.
Makosa ya Galileo yalikuwa kuunga mkono mafundisho ya Copernicus kutokana na uchunguzi alioufanya kwa darubini yake. Kwa upande wa Kanisa, uchunguzi huu ulikuwa mgumu zaidi kupambana nao, kuliko ile elimu ya kimaandishi tu ya Bwana Copernicus.
(3) Mwana Sayansi mwingine Bwana Giardino Bruno aliyeishi kati ya mwaka 1549-1600 bk, alikuwa madhbuha mwingine wa wa adhabu za kanisa dhidi ya wanasayansi. Bwana huyu alichomwa hali ya kuwa yu hai,
"Hivyo mahakama ya hukumu ya kiksrito dhidi ya wazushi wa Kidini, ilitangiza hukumu na msimao wa kanisa kuwa ndiyo ukweli. "na kusema kwamba: fikra ya kuwa Jua ndio kitovu (center) cha Ulimwengu na kuwa Jua haliizunguki dunia ni wa kijinga, kipuuzi, usio na ukweli hata kidogo,kwani, hauafikiani na na unakinzana maandishi Matakatifu , na pia fikra isemayo kuwa dunia si kitovu cha ulimwengu na kwa hiyo dunia ina lizunguka jua ni upuuzi, ni uwongo, na kwamba fikra hii inapingana na elimu ya hekima (filosofia)." (Rejea katika kitabu kiitwacho "Religion and Science".)
Kwa sababu ya kukabiliwa na mastaka na adhabu kali, Wanasayansi waliueleza Ukristo, kuwa ni "imani isiyo pendelea mambo ya kiakili na isiyopendelea mambo ya Kisayansi; na kwamba ukiristo ni kitu kirudishacho nyuma maendeleo ya binaadamu."
Jambo la kustaajabisha ni kuwa wameichukulia kila dini kwa ujumla kuwa ni sawa na Ukristo.
Hivyo hoja ya kwanza si sahihi kwani imetazama dini moja na kuhukumu dini zote. Yamkini ikawa sahihi kwa dini ya kiksrito ila si sahihi kwa dini nyingine kama Uyahudi, Uislamu na nk.
Hoja ya pili: isemayo kuwa Dini ni dawa iliyogunduliwa na mabepari ili kuwatuliza watu wa tabaka la chini, na kuwafanya watosheke na hali yao hiyo ya kimaskini, si sahihi na inapingana hata na historia kwani historia inatuonyesha kuwa dini haikuanzishwa na mabepari bali ili letwa na manabii na kwamba moja kati ya mafunzo ya dini ilikuwa ni kupinga dhulma na kuleta usawa, jambo ambalo linakinzana kabisa na malengo ya mabepari.
Hivyo Dini inaumuhimu mkubwa sana kwa wanadamu, kwani inawafunza njia sahihi za maisha, inawafunza na kuwakumbusha kulinda haki za binadamu na hatimaye kuwa na maisha ya utulivu wa kimwili, kiroho na kiakili.