Main Title

source : ABNA
Jumanne

7 Januari 2020

07:43:54
1000132

Mamia ya waumini wa Kikristo mjini Aleppo nchini Syria, wamekusanyika Katika kanisa lao kwa ajili ya kuomboleza na kukumbuka kifo cha Qasem Soleimani.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na Mchungaji Ibrahim Nasir, ambaye ni kiongozi wa Kanisa hilo akiuambia umati huo kwamba Qasem Soleimani hakuwa na lingine zaidi ya kusimama na kupambana na mabepari, jambo ambalo hata Masihi (Yesu) alikuwa akilifanya.

“...Leo hii jambo ambalo linafanywa na Qasem Soleimani ni jambo la kusimama kidete, kama ambavyo baba Masihi alikuwa akifanya, si kwa jambo lingine bali ni dhidi ya nguvu za kisiasa zenye kutaka kuchukua uhuru wa wengine....” alisema mchungaji Ibrahim.

Waumini wa Aleppo ni waumini ambao wamekuwa wakishuhudia mara kwa mara matatizo ya kunyanyaswa kiitikadi na vikundi vyenye kuungwa mkono na nguvu za mabepari, ambapo mwaka 2012 waliwahi kushambuliwa na hata kutaka kutolewa kwa nguvu na majeshi ya NATO.

mwisho/290