Main Title

source : ABNA
Jumatano

29 Januari 2020

10:09:24
1006228

Ni mara kadhaa Rais wa Marekani amekuwa akiashiria kusimama pamoja na wananchi wa taifa la Iran, lakini swali la kujiuliza hapa ni kwamba kwa kiasi gani na vipi maneno haya yanaendana na hali halisi?.

Shirika la habari la Ahlubayt (as) ABNA:

Ni mara kadhaa Rais wa Marekani amekuwa akiashiria kusimama pamoja na wananchi wa taifa la Iran, lakini swali la kujiuliza hapa ni kwamba kwa kiasi gani na vipi maneno haya yanaendana na hali halisi?.

Ni mara ngapi Trump alinukuliwa akiliita taifa hilo kuwa ni taifa la Magaidi?, ni vikwazo vya aina gani ambavyo ameliwekea taifa hilo hasa baada ya kujitoa katika makubaliano ya nyuklia?.

Wananci wamezidi kufariki mahospitalini kutokana na ukosefu wa dawa, leo hii Iran ni katika nchi ambazo wananchi wake hawana haki ya kupata visa za kuingia Marekani, kwa amri ya Marekani viongozi wa juu wa Jeshi la Iran wanauwawa, na pale ambapo Iran inapojaribu kujibu mapigo hayo basi jibu la vitisho vya kushambulia vitua zaidi ya 52 vya kitamaduni ndilo huwa mstari wa mbele.

Je, ni kweli Trump yupo pamoja na Wairani au yupo kwa ajili ya kuwaangamiza?!.