Main Title

source : ABNA
Jumatatu

24 Februari 2020

06:48:21
1012761

Video: Mauaji ya kinyama dhidi ya vijana wa Kipalestina

Kwa kile kinachoaminika kuwa na mwendelezo wa unyama na ukatili dhidi ya Wapalestina, Wanajeshi wa Israel siku ya jana (Jumapili) wameendeleza mauaji hayo yaliyosababisha kifo cha kijana mmoja na wengine wanne kujeruhiwa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA:

Kwa kile kinachoaminika kuwa na mwendelezo wa unyama na ukatili dhidi ya Wapalestina, Wanajeshi wa Israel siku ya jana (Jumapili) wameendeleza mauaji hayo yaliyosababisha kifo cha kijana mmoja na wengine wanne kujeruhiwa.

Katika video inayoonyesha aina ya mauaji hayo, imeshuhudiwa wanajeshi hao wakitumia gari maalumu la wakandarasi (Greda) kama silaha na hatimaye kuuponda mwili wa kijana aliyepoteza maisha.

Katika kuzungumzia tukio hilo kikundi cha Jihadi cha Kiislamu cha Hamas kimesema kwamba kamwe hakitakubali Israel iendelee na vitendo vyake vya kinyanyasaji dhidi ya mataifa ya Kiarabu.

Aidha pia katika taarifa yao Hamas wamesema kuwa kitendo chochote chenye ishara ya kuharibu amani ya Ghaza hakitafumbiwa macho na kwamba kisasi lazima kitachukuliwa, kama ambavyo vitisho vya maadui havitafua dafu kuelekea harakati yao hiyo.

“...Tunasema kwamba tutakata mikono ya wote waliohusika na mauaji ya vijana hawa, kama ambavyo tumefanya hivyo kwa mateka wa mwanzo, kamwe hatuwezi kuwatelekeza watu wetu...” taarifa ya wanamgambo hao ilisema.