Main Title

source : parstoday
Jumatatu

15 Juni 2020

07:58:58
1046745

Mwafrika aokoa maisha ya mzungu mwenye chuki kali za kibaguzi nchini Uingereza + Video

Kitendo cha uungwa na kiwango cha juu cha ubinadamu kilichooneshwa na rais mmoja wa Uingereza mwenye asili ya Afrika cha kuokoa maisha ya mzungu mwenye chuki kali za kibaguzi wakati wa ugomvi huko mjini London Uingereza, kimevigusa sana vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Vyombo vya habari likiwemo gazeti la The Guardian la nchini Uingereza vimeiakisi kwa wingi mno habari hiyo na kuonesha jinsi Muingereza huyo mwenye asili ya Afrika alivyoonesha uungwana wa hali ya juu katika tukio hilo.

Mzungu huyo mwenye misimamo mikali na ya kufurutu ada anayechukia sana wageni hasa Waafrika, alikwenda kwenye maandamano hayo kupigana na waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi na alihatarisha vibaya maisha yake katikati ya kundi hilo la watu wenye hasira.

Akitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, Patrick Hutchinson aliyembeba mzungu huyo ili kuokoa maisha yake anasema: "Maisha yake yalikuwa hatarini, hiyo niliamua tu kwenda, nikamtwaa na kumuweka mabegani na kukimbia naye upande walipokuwepo polisi."

Vile vile amegusia jinsi polisi mzungu alivyomuua kikatili mchana kweupe na kwa damu biridi kabisa, Mmarekani Mwafrika anayejulikana kwa jina la George Floyd huko Minneapolis nchini Marekani na kusema, kama wale maafisa wengine wa polisi waliokuwepo sehemu ile, wangeliingilia kati basi leo George Floyd angelikuwa bado yuko hai.

Kiujumla amesema, hata kama na yeye asingelichukua uamuzi huo wa kuokoa maisha ya mzungu huyo bila ya kujali chuki zake za kikabila, basi angeliweza kuuliwa na watu wenye hasira.

Amesema, wakati kama ule mtu hutakiwi kufikiria hatari zinazokukabili, unachotakiwa ni kutekeleza wajibu wako. Maandamano makubwa ya kupinga ubaguzi wa rangi yangali yanaendelea, si nchini Marekani tu, bali pia katika nchi mbalimbali duniani licha ya kwamba baadhi ya wazungu wabaguzi wenye chuki za kikabila wakionesha waziwazi kuunga mkono mauaji hayo ya kikatili. 

342/