Main Title

source : parstoday
Alhamisi

25 Juni 2020

13:06:59
1050274

Jeshi la Anga la Iran lapokea ndege za kivita za 'Kauthar'

Kikosi cha Anga cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimepokea ndege tatu za kivita aina ya 'Kauthar' zilizotengenezwa na wataalamu wa humu nchini.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Amir Hatami na maafisa wa wengine wa ngazi za juu wa majeshi ya Iran wamehudhuria hafla iliyofanyika mapema leo Alkhamisi ya kupokezwa ndege hizo za kijeshi za 'Kauthar' zilizozalishwa hapa nchini kwa Jeshi la Anga la Iran.

Ndege hizo zina uwezo mkubwa wa kutekeleza operesheni za mashambulizi na zitatumika pia katika kuwapa mafunzo marubani wa kijeshi wa taifa hili.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilianza kuzalisha kwa wingi kizazi cha nne cha ndege za kisasa za kivita za 'Kauthar' mwezi Novemba mwaka 2018.

Ndege hizo ina uwezo mkubwa na ina mfumo automatiki na wa kidijitali wa kizazi cha nne. Ndege hiyo ina mfumo maalumu wa silaha na mfumo wa rubani wa HUD kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa kulenga shabaha.

Ndege ya kivita ya 'Kauthar' inayopaa kwa mwendo wa kasi zaidi inatazamiwa kutoa mchango mkubwa katika kuihami anga ya Jamhuri ya Kiislamu.


342/