Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

2 Januari 2021

08:36:50
1102151

Brigedia Jenerali Qaani: Njia ya Kikosi cha Quds haitabadilishwa kwa ushetani wa Marekani

Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) nchini Iran amesema kuwa Shahidi Qassem Soleimani ni shujaa wa taifa la Iran, Umma wa Kiislamu na vilevile shujaa wa kuyashinda madola ya kibeberu na kuongeza kuwa, njia ya Kikosi cha Quds na wanamuqawama haiwezi kubadilishwa kwa ushetani wa Marekani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Brigedia Jenerali Esmail Qaani ameyasema hayo leo Ijumaa hapa mjini Tehran katika shughuli ya mwaka wa kwanza wa kukumbuka mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Abu Mahdi al Muhandis na wenzao kadhaa. Amesisitiza kuwa adui alikuwa akimsaka kwa udi na uvumba Luteni Jenerani Soleimani kwa kipindi cha miaka 30 na kuongeza kuwa: Mtu huyu punguani (Donald Trump) ndiye muovu na mtenda jinai mkubwa zaidi duniani ambaye hajali mpaka wa aina yoyote; na kutokana na ushawishi wa ushetani wa utawala haramu wa Israel na utawala wa Saudia, alitenda jinai isiyo na mfano duniani ambayo haijafanywa kwa shakhsia yeyote wa kisiasa na kijeshi katika zama hizi.

Brigedia Jenerali Qaani amewaambia Wamarekani kuwa: Wale waliotenda jinai hiyo wanapaswa kuelewa kwamba, wamefanya jambo ambalo popote pale watakapokuwa katika dunia hii atatokeza mtu atakayetoa jazaa na malipo stahiki kwa waovu hao. 

Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Kwa jinai hiyo mliyofanya mmetengeza kazi nyingine kwa watu huru duniani, na eleweni kwamba, hata ndani ya majumba yenu nyinyi wenyewe yumkini akajitokeza mtu atakayetoa jibu kwa jinai na uhalifu huo. 

Brigedi Jenerali Qaani ameashiria wahka na woga wa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mipaka ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kusema: Syria inaendelea kusimama kidete na hii leo karibu ardhi yote ya nchi hiyo imekombolewa; Iraq ya jihadi inaendelea kusimama imara na Yemen iliyodhulumiwa bado inapiga hatua madhubuti; hii ndiyo njia ya Shahidi Soleimani ambayo itaendelea kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu. 

Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Abu Mahdi al Muhandis ambaye alikuwa naibu mkuu wa harakati ya wananchi wa Iraq ya al Hashul Shaabi na wenzao 8 waliuawa shahidi tarehe 3 Januari mwaka 2020 kwa shambulizi la anga la wanajeshi magaidi wa Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq. Jenerali Soleimani alikuwa Iraq kwa mwaliko rasmi wa aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo. 

342/