Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

9 Januari 2021

14:54:49
1104437

Iran Yazindua kituo kikubwa cha chini ya ardhi cha makombora Ghuba ya Uajemi + VIDEO

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limezindua kituo kikubwa na cha kistratijia cha makombora chini ya ardhi katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sherehe za uzinduzi huo zimefanyika Ijumaa ya leo na kuhudhuriwa na Meja Jenerali Hussein Salami Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). Akizungumza katika uzinduzi huo, Meja Jenerali Salami amesema mantiki ya IRGC ya kulinda mamlaka ya kujitawala, uhuru na mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu inazidi kupata nguvu.

Aidha amesema kituo hicho kikubwa cha makombora ya kistratijia cha chini ya ardhi ambacho kinamilikiwa na Kikosi cha Majini cha IRGC ni kati ya vituo kadhaa vya kistratijia vya IRGC vyenye maghala makubwa ya makombora.

Amesema makombora hayo yana uwezo wa kuruka mamia ya kilomita na yana ustadi mkubwa wa kulenga shabaha na kuharibu kabisa eneo linalolengwa sambamba na kukwepa rada za maadui.

Meja Jenerali Salami amesema Iran haina budi ila kuimarisha uwezo wake wa kujihami ili kukabiliana na njama za ubeberu za maadui.

Aidha  amesema hata kabla maadui hawajasonga mbele katika chokochoko zao, watazuiwa na vijana mashujaa na wenye uwezo mkubwa wa Iran.

342/