Main Title

source : ABNA
Jumanne

10 Oktoba 2023

13:48:53
1399634

Video| Sherehe ya kuzaliwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) ilifanyika katika seminari ya Sayyidah Sukaina (AS) nchini Uganda.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bait (A.S) - ABNA - limeripoti kuwa, katika mnasaba wa kuzaliwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) na Imam Ja'afar Sadik (AS), kulifanyika sherehe maalum katika shule hiyo na seminari ya Sayyidah Sukaina (AS) huko Kampala, mji mkuu wa Uganda.

Ayatullah Ramazani mkuu wa baraza la dunia la Ahlul Bayti (AS) ambaye alikuwa mgeni mkuu wa maadhimisho haya amepongeza shughuli za mkuu wa taasisi hiyo Sheikh Husain Al-Awali katika kukuza na kufafanua mafundisho ya Ahlul Bayti (AS). Shule ya Sayyidah Sukainah (AS) na seminari nchini Uganda ina idara tofauti ikiwa ni pamoja na vituo vya watoto yatima