Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Raia wa Jordan walifanya maandamano makubwa katika mji wa "Irbid" kuunga mkono Muqawamah wa Palestina na kulaani Mauaji ya Shahidi "Ismail Haniyeh" yaliyofanywa Utawala Haram wa Kizayuni.
Waandamanaji hao wa Jordan walipiga nara zao dhidi ya utawala wa Kizayuni na jinai zake wakisisitiza kuendelea njia ya Shahidi Haniyeh na Muqawamah dhidi ya utawala huo ghasibu.
Wakati huo huo jana, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan, Ayman al-Safadi, alitangaza kuwa, utawala wa Kizayuni umekwamisha juhudi za pande za upatanishi za kuanzisha usitishaji vita huko Ghaza; na hilo ni kwa sababu ya kitendo chao cha kumuua Shahidi Ismail Haniyeh.
Al-Safadi alitangaza siku ya Alhamisi kwamba Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kuchukua hatua kwa njia ambayo itazuia uchokozi wa utawala wa Israel.