Main Title

source : abna.ir
Jumapili

12 Oktoba 2014

18:40:58
643949

Siku ya Ghadir

Tukio la hija ya mwisho ya Mtume Muhammad s.a.w

Ghadir

Hijja hii ilihudhuruwa na maswahaba wengi sana, inasemekana kuwa idadi yao ilikuwa takriban watu laki moja na ishirini na nne elifu (124000), watu hawa katika siku ya jummamosi tarehe 24 mwezi wa Dhilqa’adah wakiwa sanjari na mtume Muhammad s.a.w waliongozana kuelekea katika mji mtukufu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya hijja.

Katika mwaka wa kumi hijria, ambao ni mwaka wa mwisho wa maisha ya mtume Muhammad s.a.w aliazimu kwenda Makka kufanya hijja ya mwisho.

Mtume Muhammad s.a.w aliwa amuru maswahaba zake, waungane nae katika safari hii tukufu ya hija ya mwisho ya mtume Muhammad s.a.w, ambapo hijja hii inafahamika kama hija ya kuagana.

Hijja hii ilihudhuruwa na maswahaba wengi sana, inasemekana kuwa idadi yao ilikuwa takriban watu laki moja na ishirini na nne elifu (124000), watu hawa katika siku ya jummamosi tarehe 24 mwezi wa Dhilqa’adah wakiwa sanjari na mtume Muhammad s.a.w waliongozana kuelekea katika mji mtukufu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya hijja.

Watu wengine kutoka Makka,Yemen na sehemu nyingine pia walihudhuria katika hijja hii ya kuagana na mtume Muhammad s.a.w, ama hakika hii ilikuwa ni Hija ya pekee, ambayo haijawahi kutokea katika zama hizo na haitakuja kutokea.

Katika hijja hii mtume alitoa nasaha muhimu na mafunzo ya hijja kwa mahujjaji walio kuja ili wafundishe kizazi kijacho, mpaka hivi sasa nasi tunakwenda Makka kuhiji kwa kufuata desturi na mafunzo hayo ya mtume Muhammad s.a.w.

Baada ya ibada ya hijja kwisha mtume Muhammad s.a.w na mahujaji wengine walianza safari za kurudi kwao, walipofika katika sehemu iitwayo Ghadir khum, mtume aliwaambia watu wasimame.

Ghadir khum ni sehemu iliyopo kusini mwa Madina na kaskazini mwa Makka, sehemu hii pia ni njia panda inayokusanya njia za Madina, Misri na Iraq.

Mtume aliwaambia watu wasimame katika sehemu hiyo kwa kuwa alipokea ujumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, ujumbe huu alitakiwa kuufikisha kwa watu wake, na hii ndio sababu iliyomfanya awasimamishe waliokuwa karibu na kuamuru warudi walio kuwa mbali.

Kipindi hicho ilikuwa ni kipindi cha joto, jua lilikuwa ni kali na lenye kuchoma kweli kweli, lakini kwa kuwa ilikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu, kiumbe na mja wa ukweli wa Mwenyezi Mungu hakuwa na hiari ila kutii amri ya Mwenyezi Mungu na agizo la mtume Muhammad s.a.w.

Malaika Jibril alipewa ujumbe na Mwenyezi Mungu, amwambie na kumsisitiza mtume Muhammad s.a.w  kwamba afikishe ujumbe aliyopewa na Mola wake:  ujumbe huu unapatika katika suratul Maida aya 67:

َا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ

Aya hii inamsititiza mtume awaambie watu, ujumbe aliopewa na Mwenyezi Mungu mtukufu, lakini mtume alikuwa na hofu kuhusu mapokeo, Je watu wataupokea vipi ujumbe huo?

Aya hii inamwamuru mtume Muhammad s.a.w afikishe ujumbe huo, na kama hatofikisha basi utume wake wote utakuwa ni kazi bure, pia aya hii inamwambia asihofu watu kwani Mwenyezi Mungu mtukufu atamkinga na shari za watu.

Je ujumbe huo ni ujumbe gani hata ukatiliwa maanani kiasi hiki?

Ndugu msomaji kama utakuwa makini na mada hii, hapo awali tulieleza kuwa hii ni hija ya mwisho ya mtume Muhammad s.a.w  na pia ndio hija ya kuagana na mtume Muhammad s.a.w kwani baada ya hapo mtume aliiaga dunia.

Ukweli ni kwamba mtume alipewa ujumbe ambao alitakiwa awafikishie waislamu ili wasije wakatofautiana baada ya kifo chake.

Maswahaba waliamuandalia membari mtume Muhammad s.a.w, naye alipanda membari na kuwa  fikishia watu ujumbe aliosisitizwa na Mwenyezi Mungu aufikishe kwani ni ujumbe muhimu saana.

Siku hii ilikuwa ni tarehe 18 mwezi wa Dhulhaj mwaka wa 10 hijiria sawa na tarehe 10 March (mwezi wa tatu )  mwaka 632 AD. Ujumbe huu unaonekana ni ujumbe mzito kwani pamoja na joto kuwa kali mtume hakujali bali aliazimia kufikisha ujumbe huo muhimu.

 Mtume Muhammad s.a.w alipanda juu ya membari aliyoandaliwa na maswahaba, na aliongea nao kwa kuanza kumshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu.

Kisha akawaambia: Enyi watu sidhani kama tunaonana na kukutana tena baada ya makutano yetu haya, Je mnakubali kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja na mimi ni mtume wake?

Watu wakajibu: ndiyo.

Kisha akasema: Yeyote anayeamini kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja na mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu, anatakiwa amini kwamba baada ya kifo changu Ali bin Abi Twalib ndiye kiongozi wa uislamu.

Kisha mtume Muhammad s.a.w akamaliza kwa kusema: Eeeh Mwenyezi Mungu, mnusuru mwenye kumnusuru Ali, na mfanyie uadui mwenye kufanyia uadui Ali. Eeh Mwenyezi Mungu shuhudia kuwa nimefikisha ujumbe ulonipatia.

Kisha mtume aliwataka watu waliopata ujumbe huo kuwafikishia wasio upata.

Baada ya hapo malaika Jibril alimjia mtume Muhammad s.a.w na kumfikishia ujumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, ujumbe huu unapatikana katika suratul Maida aya ya sita na ujumbe huu unasema kwamba:

الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini.

Ukhalifa wa Ali bin Abitwalib ndio ujumbe ambao mtume Muhammad s.a.w alikuwa anahofia kuufikisha,

Hivyo siku hii inajulikana kama siku ya Ghadir, siku hii ni siku ambayo mtume alimtangaza kiongozi atayeongoza umma wa kiislamu baada yake, siku hii ni siku ambayo dini ya Uislamu ilikamilika na kuwa dini timamu.

Siku hii ni siku muhimu sana katika historia ya uislamu, siku hii ni sikukuu na inasherekewa na waislamu wengi hususan waislamu wa dhehebu la Shia.

Swali la kujiuliza ni kwamba, Je baada ya kufariki mtume Muhammad s.a.w Ali bin Abitwalib alipewa madaraka aloachiwa na mtume? Je ni watu wote walimfuata? Kwanini wengine hawamkumfuata?  Waliomfuata ni kina nani? Kwanini watu waliweza kusahau maagizo ya mtume na kupuuzia tukio zima la Ghadir?