Main Title
15 Mei 2024
Katibu Mkuu wa UN alaani mauaji ya wafanyakazi wa afya huko Rafah
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelaani mauaji na kujeruhiwa kwa maafisa wa afya wa Umoja wa Mataifa huko Rafah kusini mwa ukanda wa Gaza.
15 Mei 2024
IDMC: Kuna ongezeko kubwa la ukimbizi wa ndani unaosababishwa na migogoro duniani
Ripoti mpya ya Kituo cha Ufuatiliaji wa Ukimbizi wa Ndani (IDMC) inaonyesha kuwa migogoro na ghasia duniani zimesababisha ongezeko lisilo na kifani la idadi ya wakimbizi wa ndani kufikia mwisho wa 2023.
15 Mei 2024
Uchunguzi wa Independent: Biden anahusika katika mateso ya njaa ya watu wa Gaza
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Uingereza la The Independent unasema kuwa, Rais wa Marekani, Joe Biden, anahusika katika baa la njaa linalowatesa raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
15 Mei 2024
Iran: Haki za binadamu za Marekani na Israel ni pande mbili za sarafu moja
Ali Kanani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema haki za binadamu za Marekani na Israel ni pande mbili za sarafu moja kwani zote zinakiuka pakubwa haki za binadamu dhidi ya mateka na wafungwa, moja huko Negev na nyingine huko Guantanamo na Abu Ghraib.
15 Mei 2024
"Mauaji ya watoto 15,000 wa Gaza yanaashiria mwisho wa Israel"
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hakuna shaka kuwa mauaji ya watoto zaidi ya 15,000 wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza itakuwa chachu ya kuharakisha mchakato wa kuporomoka na kusambaratika utawala wa Kizayuni wa Israel.
15 Mei 2024
Sera za Iran kuhusu nishati ya nyuklia hazijabadilika
Nasser Kanani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alitangaza Jumatatu 13 Mei kwamba, sera za nyuklia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hazijabadilika.
15 Mei 2024
Balozi wa Russia UN: Mashambulizi ya Magharibi dhidi ya Yemen ni kinyume cha sheria
Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa mashambulizi ya muungano wa nchi za Magharibi unaoongozwa na Marekani dhidi ya Yemen yamekiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa na hayana uhalali wowote.
15 Mei 2024
Marekani na Uingereza zashambulia tena uwanja wa ndege wa al Hudaidah huko Yemen
Ndege za kivita za Marekani na Uingereza kwa mara nyingine tena zimeushambulia uwanja wa ndege wa kimataifa wa al Hudaidah huko Yemen.
15 Mei 2024
Wapalestina elfu 10 wangali chini ya vifusi
Taasisi ya Ulinzi wa Raia ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa Wapalestina elfu 10 bado wapo chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa katika mashambulizi ya jeshi la Israel.
15 Mei 2024
Msemaji wa UNRWA atahadharisha kuhusu hali ya mji wa Rafah
Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) ameitaja hali ya mji wa Rafah huko kusini mwa Ukanda wa Gaza kuwa sawa na mji uliotelekezwa uliosalia magofu.
15 Mei 2024
ICJ itasikiliza kesi kuhusu uvamizi wa Israel dhidi ya Rafah
Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) itafanya vikao kujadili hatua mpya za dharura kuhusu uvamizi wa Israel katika mji wa kusini wa Rafah katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.
15 Mei 2024
Maelfu ya Wapalestina waandamana katika kumbukumbu ya siku ya Nakba
Maelfu ya wananchi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu wameandamana kwa mnasaba wa Siku ya Nakba ambayo inakumbusha uvamizi, mauaji ya kimbari, ukatili na jinai za Wazayuni katika ardhi za Wapalestina.
14 Mei 2024
Balozi wa Yemen nchini Iran: Mkutano wa Tehran utaleta maelewano kati ya Iran na Waarabu
Balozi wa Yemen nchini Iran amesema kuwa Mkutano wa Mazungumzo ya Iran na Waarabu uliofanyika mjini Tehran chini ya anwani "Kwa ajili ya Ushirikiano na Maelewano" utaliimarisha taifa la Palestina na kuboresha maelewano kati ya Iran, Waarabu na nchi mbalimbali.
14 Mei 2024
Familia za wanajeshi waliouawa zamshambulia Waziri wa Usalama wa Israel
Familia za wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliouawa vitani Ukanda wa Gaza zimemshambulia Itamar Ben- Gvir Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni.
14 Mei 2024
Nasrullah: Wanajeshi 1,500 wa Israel wameuawa tangu kuanza vita vya Gaza
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema wanajeshi 1,500 wa Israel wameuawa tangu kuanza vita vya utawala huo haramu dhidi ya Gaza, jambo ambalo limeyalazimu makundi ya muqawama katika eneo la Magharibi mwa Asia, ikiwemo Hizbullah, kuanzisha mashambulizi dhidi ya Israel ili kuilazimisha kukomesha vita hivyo.
14 Mei 2024
Sababu za kushindwa mazungumzo ya kusitishwa vita vya Gaza
Khalil al-Hayya, Naibu Mkuu wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, amefafanua jinsi utawala wa Kizayuni wa Israel ulivyovuruga mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza na kubadilishana mateka.
14 Mei 2024
Yemen yaonya inaweza kulenga shabaha za adui 'ambazo hawezi hata kuzifikiria'
Jeshi la Yemen limeonya kuwa huenda likazidisha mashambulizi yake ya kuiunga mkono Palestina iwapo utawala wa Israel utaendelea na vita vyake vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.
14 Mei 2024
Amir wa Qatar na Waziri Mkuu wa Malaysia wajadili uhusiano wa pande mbili na hali ya Gaza
Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani amekutana na kufanya mazungumzo na Anwar Ibrahim Waziri Mkuu wa Malaysia katika mji mkuu wa nchi hiyo Doha. Waziri Mkuu wa Malaysia yuko nchini Qatar kwa ziara ya siku tatu.
14 Mei 2024
Makumi ya Wapalestina wauawa katika hujuma za Israel Gaza
Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimefanya mashambulizi mapya ya anga dhidi ya maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza na kuua shahidi makumi ya Wapalestina, wakiwemo watoto wadogo na wanawake.
14 Mei 2024
Iran: Haki za binadamu za Marekani na Israel ni pande mbili za sarafu moja
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran anasema haki za binadamu za Marekani na Israel ni pande mbili za sarafu moja kwani zote zinafanya uhalifu mkubwa dhidi ya wafungwa.