Mazungumzo hayo ya jana kati ya Amir wa Qatar na Waziri Mkuu wa Malaysia yamegusia uhusiano wa pande mbili na njia za kuimarisha na kuendeleza uhusiano katika nyanja mbalimbali za ushirikiano na katika masuala ya kikanda na kimataifa khususan matukio ya sasa huko Ukanda wa Gaza na katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Waziri Mkuu wa Malaysia yupo ziarani Qatar huku nchi mbili zikiadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kati yazo. Hii ni ziara ya kwanza ya Anwar Ibrahim huko Qatar tangu ateuliwe mwezi Novemba mwaka 2022. Viongozi hao wawili kwa mara ya mwisho walionana mwezi uliopita mjini Riyadh Saudi Arabia. Anwar Ibrahim amefuatana na Mawaziri wa Uwekezaji, Biashara, Viwanda na Elimu ya Juu wa Malaysia katika ziara hiyo ya siku tatu nchini Qatar.
342/