Rais Raisi alifariki dunia Mwezi Mei 2024 kutokana na ajali ya helikopta akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Hossein Amir-Abdollahian, na maafisa wengine waliokuwa kwenye safari ya kikazi Kaskazini-Magharibi mwa Iran.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Marasimu ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa kishahidi kwa Rais Ebrahim Raisi na wenzake ilifanyika siku ya Alhamisi katika Uwanja wa Imam Hussein (AS) Jijini Tehran.
Tukio hilo lilihudhuriwa na maafisa waandamizi wa serikali, viongozi wa kidini, wananchi pamoja na familia za mashahidi.
Hafla hiyo ilijumuisha usomaji wa Qur’an Tukufu, maombolezo na hotuba zilizomuelezea Rais Raisi kama Kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele katika kuhudumia Taifa.
Rais Raisi alifariki dunia Mwezi Mei 2024 kutokana na ajali ya helikopta akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Hossein Amir-Abdollahian, na maafisa wengine waliokuwa kwenye safari ya kikazi Kaskazini-Magharibi mwa Iran.
Washiriki wa hafla hiyo walionyesha heshima zao kwaashahidi hao na kuahidi kuendeleza njia na maadili waliyoyasimamia katika kulitumikia Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Your Comment