-
Mwenyezi Mungu Akiwa Upande Wako, Hakuna Awezaye Kukudhuru
Lengo na makusudio ya kauli hii inayosapoti na Aya hizo Tukufu ni kuondoa hofu moyoni, kwa kutomwogopa yeyote anayenuia kuwa “juu yako” au kukudhuru kwa lolote, kwani Mwenyezi Mungu akiwa pamoja nawe, hakuna mwenye uwezo juu yako isipokuwa kwa idhini Yake.
-
Afisa wa Urusi: Marekani iache kuunga mkono wanaotaka kujitenga wa Taiwan
Afisa mmoja wa bunge la Urusi amesema kuwa Marekani na China zinaweza tu kuwa karibu ikiwa Washington itaacha kusaidia wanaotaka kujitenga wa Taiwan.
-
Afisa wa usalama wa Urusi: Zelensky lazima aishi mafichoni maisha yake yote
Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi amesema kuwa Rais wa Ukraine lazima aishi kwa siri maisha yake yote yaliyosalia.
-
Mbunge wa Belarus: Kyiv inaelekea kusambaratika kutokana na kuongeza mivutano
Mbunge mmoja wa Belarus amesema kuwa utawala wa Ukraine unaelekea kusambaratika kwa kuongeza mivutano na Moscow.
-
Trump: Mazoezi ya kijeshi ya China karibu na Taiwan hayatii wasiwasi
Rais wa Marekani amepuuzia uwezekano wa China kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya vikosi vya wanaotaka kujitenga wa Taiwan katika siku za usoni.
-
Mwitikio wa Ansarullah kwa harakati za Imarati na Saudi Arabia kusini mwa Yemen
Mmoja wa maafisa wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amejibu maendeleo ya kusini mwa nchi hiyo na harakati za Imarati (UAE) na Saudi Arabia.
-
Mamluki wa Imarati: Shambulio la Saudi Arabia nchini Yemen lilikuwa la kichokozi
Naibu Mwenyekiti wa baraza linalofungamana na Imarati (UAE) nchini Yemen ameelezea shambulio la leo la muungano wa Saudia dhidi ya Hadramout kama uchokozi.
-
Axios: Trump na Netanyahu wakubaliana kutekeleza hatua ya pili ya usitishaji vita Gaza
Tovuti moja ya Marekani imeandika kuwa Netanyahu na Trump katika mkutano wao huko Florida, licha ya tofauti ndogo za kimaoni, wamekubaliana kutekeleza hatua ya pili ya usitishaji vita huko Gaza.
-
Mwitikio wa Ansarullah ya Yemen kuhusu kifo cha kishahidi cha Abu Obeida
Ofisi ya kisiasa ya Ansarullah nchini Yemen, ikisisitiza kuendeleza njia ya mashahidi mashujaa wa upinzani, imetoa pongezi na rambirambi kwa kuuawa kishahidi kwa kundi la makamanda wa Brigedi za Al-Qassam huko Gaza katika mashambulizi ya adui wa Kizayuni.
-
Onyo la Saudi Arabia kwa Imarati (UAE): "Ondoa majeshi yako Yemen"
Kuongezeka kwa mapigano nchini Yemen na jukumu la Imarati katika kuunga mkono waasi wa kusini mwa nchi hiyo kumepelekea Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia kutoa onyo kwa Abu Dhabi.
-
Jenerali Abdollahi: Utawala wa Kizayuni unadhibiti takwimu za mapigo uliyopata
Kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya alisema: "Utawala wa Kizayuni ulipata mapigo makali sana katika vita vya siku 12, lakini utawala huo unadhibiti na kuficha takwimu za vifo na mapigo uliyopata."
-
Sa‘yi kati ya Safa na Marwa: Alama ya Imani na Nguzo Muhimu ya Hija na Umra
Aya hii tukufu inathibitisha kuwa sa‘yi baina ya Safa na Marwa ni sehemu muhimu ya ibada ya Hija na Umra, na kwamba hakuna dhambi wala lawama katika kuitekeleza. Kinyume chake, ni ibada iliyoidhinishwa na Qur’ani na kusisitizwa na Sunna ya Mtume ﷺ, na aya imekuja mahsusi kuondoa shaka na uzito uliokuwepo katika nyoyo za watu kuhusu ibada hii.
-
Trump Akiri Kushiriki katika Jinai
Kauli ya Donald Trump, rais wa Marekani, iliyokiri wazi kiwango cha msaada mkubwa wa Marekani kwa Israel, imezua mjadala mpana katika uwanja wa siasa za kimataifa. Wachambuzi wanasema kauli hiyo inaashiria ushiriki wa moja kwa moja wa Marekani katika sera na hatua zinazohusishwa na ukaliaji wa ardhi, uvamizi na ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wananchi wa Palestina, jambo lililoibua maswali mazito kuhusu uwajibikaji wa kimaadili na kisheria wa Washington mbele ya jumuiya ya kimataifa.
-
Ukraine Yashambulia Makaazi ya Putin kwa Ndege Droni 91 / Trump Ashtuka
Ikulu ya Kremlin jioni ya Jumatatu ilitangaza kuwepo kwa mawasiliano ya simu kati ya marais wa Urusi na Marekani, na kubainisha kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, alishtushwa na shambulio la ndege zisizo na rubani (droni) la Ukraine dhidi ya makaazi ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin.
-
Abu Ubaida: Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa Iliamsha Dhamiri za Ulimwengu / Hatutaweka Silaha Chini; Israel Lazima Ivuliwe Silaha +Picha-Video
Msemaji mpya wa Brigedi za Al-Qassam, katika hotuba yake ya leo usiku, pamoja na kutangaza kuuawa shahidi kwa idadi ya makamanda wakuu wa harakati hiyo, amesema kuwa wanasisitiza kwamba taifa la Palestina kamwe halitaweka silaha zake chini, na kwamba mjadala unaolenga kushughulikia au kunyang’anya silaha za Wapalestina unapaswa kukomeshwa.
-
Viongozi wa Serikali na Jeshi la Polisi Jijini Mwanza Watunukiwa Tuzo za Amani Kupitia Kamati ya Maandalizi ya Maridhiano Day 2026
Kamati ya Maandalizi ya Maridhiano Day 2026 imetoa tuzo za heshima kwa viongozi wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Jeshi la Polisi, kama ishara ya kutambua mchango wao katika kudumisha amani, mshikamano na utulivu wa kijamii. Tuzo hizo zilitolewa katika hatua inayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za serikali, vyombo vya ulinzi na jamii kwa ujumla kuelekea maandalizi ya tukio hilo muhimu la Maridhiano Day 2026.
-
Mkwamo katika Bunge la Iraq; mizani ya kisiasa yameelemea kwa Waislamu wa Kishia na Wakurdi
Wakati ambapo Waislamu wa Kisunni wameshindwa kufikia mwafaka juu ya mgombea mmoja, hatima ya urais wa Bunge la Iraq imefungamana zaidi kuliko wakati mwingine wowote na maamuzi pamoja na hesabu za kisiasa za Waislamu wa Kishia na vyama vya Kikurdi.
-
Araqchi: Umoja wa ardhi na mamlaka ya Yemen lazima vilindwe
Katika mazingira ya kuongezeka kwa mvutano wa kisiasa na kijeshi nchini Yemen, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi, amesisitiza ulazima wa kulindwa umoja wa ardhi na mamlaka ya kujitawala ya nchi hiyo, akionya dhidi ya madhara ya mgawanyiko na kuingilia masuala ya ndani. Kauli hiyo imetolewa kupitia mazungumzo ya simu na mawaziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, huku pia akigusia hali ya usalama nchini Yemen na kulaani uchokozi unaoendelea wa Israel dhidi ya Lebanon.
-
Pendekezo la utaratibu mpya wa kumchagua Rais wa Iraq kutoka kwa Masoud Barzani
Masoud Barzani amewasilisha utaratibu mpya wa kumchagua Rais wa Iraq, kwa lengo la kuimarisha mshikamano wa Wakurdi na kuimarisha nafasi yao katika wadhifa huo.
-
Kiongozi Mkuu wa Wahouthi: Hatutakubali Israel kutumia ardhi ya Somalia kama kambi ya kijeshi
Ikumbukwe kuwa, moja ya sababu kuu zinazotajwa katika hatua ya Israel kuitambua Somaliland ni nafasi ya kijiografia ya eneo hilo, ambayo inaonekana kuwa na umuhimu wa kimkakati kwa Israel katika kuendesha mashambulizi dhidi ya Wahouthi wa Yemen.
-
Zaher Al-Mahrouqi katika mahojiano na ABNA:
Mfano wa Somaliland utaenea kwa nchi nyingine / Taa ya kijani kwa hatua hii italigharimu eneo kwa gharama kubwa za kiusalama!
Mwandishi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Oman, katika mahojiano na ABNA, ameielezea hatua ya Israel ya kuitambua Somaliland kuwa ni jaribio hatari la kulazimisha uhalisia mpya dhidi ya wananchi wa Palestina. Alisisitiza kuwa uamuzi huu si tu ukiukaji wa wazi wa haki za Wapalestina, bali pia unaweza kutathminiwa kuwa sehemu ya mradi wa kuliondoa Gaza wakazi wake na kufanya uhandisi wa idadi ya watu katika eneo.
-
Macron: Paris itakuwa mwenyeji wa mkutano wa waungaji mkono wa Ukraine mwezi Januari
Rais wa Ufaransa ametangaza kuwa nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi zinazoiunga mkono Ukraine mwezi Januari.
-
Zelensky: Ukraine iko tayari kwa amani
Rais wa Ukraine, huku akitaja mazungumzo yake na Rais wa Marekani kuwa ya kuridhisha, amesema: "Ukraine iko tayari kwa amani."
-
Al-Houthi: Uwepo wa Israel huko Somaliland utakuwa lengo halali la majeshi ya Yemen
Kiongozi wa harakati ya wananchi ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa uwepo wa utawala wa Kizayuni huko Somaliland utakuwa lengo halali la vikosi vya Yemen.
-
Maandamano makubwa mjini Mogadishu dhidi ya hatua ya utawala wa Kizayuni
Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, leo umeshuhudia maandamano makubwa ya wananchi kupinga hatua ya utawala wa Kizayuni kuitambua kanda ya "Somaliland" kama mamlaka iliyojitenga na Jamhuri ya Somalia.
-
Riyadh yachukizwa na hatua ya Tel Aviv; "Netanyahu ni mwendawazimu"
Chanzo kimoja katika makao ya kifalme ya Saudia kimekosoa vikali hatua ya utawala wa Kizayuni yenye utata na kinyume cha sheria kuelekea Somaliland.
-
Tamaa ya Israel juu ya maeneo ya kimkakati ya Somaliland
Chanzo cha kijeshi cha Kizayuni kimekiri kuwa utawala wa Kizayuni una tamaa na maeneo ya kimkakati ya Somaliland.
-
Naim Qassem: Upokonyaji silaha ni mradi wa Israel na Marekani
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, katika hotuba ya kumuenzi kamanda Haj Muhammad Hassan Yaghi (Abu Salim), amesema: "Upokonyaji silaha ni mradi wa 'Israel' na Marekani."
-
Misri yasisitiza "mstari wake mwekundu" kuhusu suala la Palestina
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesisitiza mstari mwekundu wa nchi hiyo kuelekea suala la Palestina pamoja na kuendelea kwa ushirikiano na makundi ya Palestina.
-
Kufichuliwa kwa mpango wa utawala wa Julani wa kuzua machafuko nchini Syria
Chanzo kimoja cha Syria kimeashiria mpango wa utawala wa Julani wa kuvuruga maandamano ya amani nchini humo kupitia watu wenye silaha.