Shirika la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Rais wa Marekani, Donald Trump, alisifu mpango wa ndege zisizo na rubani wa Iran wakati wa mkutano uliofanyika Doha, Qatar. Trump alieleza kuvutiwa kwake na ndege hizo zisizo na rubani zinazotengenezwa nchini Iran pamoja na uwezo wake wa kiutendaji.
Rais Donald Trump alisema:
“Nilimwambia mmoja wa wawakilishi wa kampuni ya Marekani kuwa ninahitaji idadi kubwa ya ndege zisizo na rubani. Nchini Iran, wanatengeneza ndege nzuri sana zisizo na rubani, na gharama ya kutengeneza kila moja ni kati ya dola 35,000 hadi 40,000.
Baada ya wiki mbili, kampuni hiyo iliniletea ndege isiyo na rubani ambayo gharama yake ilikuwa dola milioni 41.*
Nikawaambia: Hili siyo nililokusudia. Nilikuwa nazungumzia ndege isiyo na rubani isiyozidi gharama ya dola 35,000 hadi 40,000...
Ndege hizi (za Iran) ni nzuri sana, za kasi, hatari na za kutisha.”
Your Comment