Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema kuwa Iran, hii ndiyo ustaarabu wa kale zaidi unaoendelea duniani, na daima imesimama imara mbele ya dhoruba za historia. Taifa hili, kwa roho kuu na azma isiyokoma, mara nyingi limethibitisha kwamba haliinamii mbele ya wavamizi; na leo pia limesimama kwa heshima mbele ya wanyakuzi, likitegemea nguvu ya imani na mshikamano wa kitaifa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Washington haina haki ya kulazimisha siasa za nje za Iran, na kuitaka kusimamisha mara moja mauaji yake kwa watu wa Yemen.