Marekani
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani atazuru Qatar kesho
Gazeti la Washington Post, likinukuu maafisa wawili wa serikali ya eneo hilo, limeripoti kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anatarajiwa kufanya ziara nchini Qatar kesho, siku ya Jumanne.
-
Onyo kutoka kwa Kiongozi wa Ansarullah:
Kiongozi wa Ansarullah wa Yemen, akifichua ukubwa wa mauaji ya kimbari na uharibifu wa miundombinu huko Gaza, ametaja pia mipango ya upanuzi ya utawala wa Kizayuni katika eneo la kikanda, ikiwemo Lebanon, Syria na uvamizi wa hivi karibuni dhidi ya Qatar. Ameitaja Marekani kuwa mshirika katika uhalifu huu na kusisitiza kuendelea kwa mapambano na mshikamano wa Kiislamu katika kukabiliana na uchokozi huu.
-
Mwanamke Mshirika wa Harakati za Kiislamu kutoka Iraq katika mahojiano na Abna: (Sehemu ya Pili)
Ni nani wanaopinga umoja kati ya Iran na Iraq? / Macho ya Marekani na Israel yako kwenye mapato ya mafuta ya Iraq
"Zainab Basri alisema: Baadhi ya wanasiasa wa Kurdistan ya Iraq, na kwa ujumla makundi ya kisiasa yanayohusiana na Marekani na nchi za Kiarabu za Ghuba, hawapendezwi na uhusiano wa Iraq na Iran..."
-
Makala Maalum | Uso Halisi wa Marekani – Donald Trump Afichua Uso wa Kweli wa Marekani - Sura ya Ubeberu Bila Kivuli!
Donald Trump kama Mwakilishi wa Wazi wa Utawala wa Marekani, Afichua Uso Halisi wa Taifa Hilo Donald Trump, aliyekuwa rais wa Marekani, alijitokeza kama mwakilishi wa bila kificho wa watawala wa Marekani, na kupitia matendo yake, aliweka wazi sura halisi ya historia na utambulisho wa nchi hiyo. Kwa hatua yake ya kubadili jina la "Wizara ya Ulinzi" kuwa "Wizara ya Vita", Trump alifichua ukweli kwamba Marekani haiko tena tayari kujificha nyuma ya maneno ya "ulinzi" na "usalama wa kimataifa". Badala yake, alionyesha kuwa taifa hilo sasa linataka kujenga dunia mpya inayozingatia sheria ya vita, si sheria za haki za binadamu au amani ya kimataifa.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Lebanon katika mahojiano na ABNA:
"Baada ya kuondolewa kwa silaha za Hizbullah, hakuna dhamana ya kulinda Lebanon dhidi ya adui msaliti"
Adnan Mansour: Je, viongozi rasmi wa Lebanon wanaweza kusimama dhidi ya Marekani na kulinda maslahi ya Lebanon na hatari za kuondolewa kwa silaha? Nani atakayebaki Lebanon kupambana na uvamizi wa Israel? Je, jeshi la Lebanon linaweza kukabiliana na uvamizi peke yake? Kamwe.
-
Raia wa Marekani katika mahojiano na ABNA:
Watu wa dunia wako upande wa Iran, vyombo vya habari vya Magharibi vinaeneza uongo / Kisa cha ushauri wa Hajj Qasim kwa Shahidi Fakhrizadeh
"Muhammad" raia wa Marekani alisema: Ninawaambia watu wa Iran; watu wa dunia wako pamoja nanyi na vyombo vya habari vya Magharibi ukweli wanauonyesha kwa namna tofauti"
-
(Radi amali) Mwitikio wa Maduro kwa Kupelekwa kwa Manowari za Marekani Venezuela
Rais wa Venezuela ameikosoa hatua ya Marekani ya kupeleka manowari tatu za kivita karibu na pwani ya nchi yake, akitaja kitendo hicho kuwa ni “uvamizi wa kigaidi wa kijeshi, usio halali na kinyume cha sheria.”
-
“Ushirikiano wa Kutekeleza Mpango wa Marekani na Israel” / Je, “Vita kama vya Karbala” vya Hezbollah Viko Mbele
Beirut – Baadhi ya wanasiasa na wabunge wa Lebanon wamewasilisha malalamiko rasmi dhidi ya Sheikh Naeem Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah, baada ya hotuba yake ya hivi karibuni aliyoituhumu serikali ya Lebanon kwa kutaka kuisalimisha nchi mikononi mwa Israel.
-
Kuanza kwa Mchakato wa Kuondoka Kikamilifu kwa Vikosi vya Marekani kutoka Baghdad kuelekea Erbil Mwezi Septemba
Chanzo cha serikali ya Iraq kimetangaza kuwa vikosi vya Marekani vitaanza mchakato wa kuondoka kikamilifu mjini Baghdad kuanzia mwezi Septemba 2025 na kuhamia Erbil, mji mkuu wa eneo la Kurdistan nchini Iraq.
-
Sayyid Abdulmalik al-Houthi: Kuondoa Silaha za Mapambano ya Muqawama Ni Kufuata Mpango wa Kizayuni
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen, Sayyid Abdulmalik al-Houthi, amesema kuwa kuondoa silaha za mapambano ni sehemu ya mpango wa wazi wa Marekani na Israel wa kudhoofisha mataifa ya eneo hili.
-
Mmiliki wa Mawkibu Muiraq Katika Mahojiano na ABNA:
Arubaini ni fursa yenye thamani kubwa ya kubainisha uhalisia wa Jamhuri ya Kiislamu na tabia ya kinyama ya Israel
Mmiliki wa Mawkibu kutoka Iraq, akisisitiza umuhimu wa Jihadi ya Kuelimisha katika siku za Arubaini ya Imam Hussein (a.s), amesema kuwa siku hizi ni fursa muhimu ya kuwapa uelewa mataifa mbalimbali.
-
Marekani Yapongeza Uamuzi wa Baraza la Mawaziri wa Lebanon wa Kulazimisha Udhibiti wa Silaha Mikononi mwa Serikali
Mjumbe wa Marekani afurahishwa na hatua ya baraza la mawaziri la Lebanon dhidi ya silaha za Muqawama.
-
Jeshi la Mapinduzi la Iran Laonya Marekani na Israel: Jibu Litakuwa Kali Mno Kuliko Mnavyodhani
Iran iko tayari kwa Operesheni Kubwa Dhidi ya Wachokozi kwa muda wowote ule.
-
Shinikizo la Marekani kwa Umoja wa Mataifa Kuhusu Kuondoa Jina la Abu Muhammad al-Julani Kwenye Orodha ya Vikwazo vya Baraza la Usalama
Marekani imeanza kuiwekea shinikizo Umoja wa Mataifa ili kuondoa vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama dhidi ya Ahmad al-Shara, anayejulikana kwa jina la Abu Muhammad al-Julani, mkuu wa serikali ya mpito ya Syria na kiongozi wa kundi la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS).
-
Trump adai: Ninashughulikia mpango wa kuwafikishia chakula watu wa Ukanda wa Gaza
"Nipo katika hatua ya maandalizi ya kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa watu wa Gaza"
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran | Atoa Onyo kwa Marekani : "Hatutavumilia ukiukwaji wa sitisho la mapigano, Sisi sio kama Lebanon"
Kauli hii ni onyo kali kwa Marekani na washirika wake dhidi ya uvunjaji wowote wa makubaliano ya amani au usitishaji wa mapigano katika muktadha wa mvutano wa kijeshi unaoendelea katika eneo.
-
Jeshi la Yemen Latangaza Awamu ya Nne ya Kufunga Njia za Baharini, Latoa Onyo kwa Ndege Zinazosaidia Israel
Ndege yoyote, iwe ya kijeshi au kibiashara, itakayojihusisha na shughuli za kusaidia Israel, tutaiangamiza. Itaingia kwenye historia.
-
Rais wa Iran: Mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran Yameleta Umoja wa Kitaifa Usio na Mfano
"Leo tunashuhudia kwa macho yetu kuwa kila Muirani - awe ni mfuasi wa Serikali au mpinzani wake - amekuwa sauti moja katika kutetea hadhi, uhuru, na mamlaka ya nchi yetu".
-
Wataalamu wa Kieneo katika Mahojiano na ABNA: Njaa ya kimfumo dhidi ya watu wa Gaza ni uhalifu usio na kifani na doa la aibu juu ya uso wa Binadamu
Jinai za uharibifu kamili wa ardhi, watu na kila dalili za maisha katika ardhi za Palestina inayokaliwa kwa mabavu (na Utawala wa Kizayuni) zinaakisi matamanio ya jeshi la Netanyahu kuwa tawi la uhalifu wa kimataifa katika ardhi za Kiislamu.
-
Tamko la Maulamaa 100 wa Ulimwengu wa Kiislamu: Trump na Netanyahu ni Maadui wa Mwenyezi Mungu
Marekani na Israel ni wakiukaji wakubwa wa Haki za Binadamu na waendelezaji wa vita visivyo halali dhidi ya Mataifa ya Kiislamu (Palestina, Yemen, Lebanon, Iraq, Iran n.k).
-
Marekani Yarejea Katika “Sheria ya Msituni” - Jarida la Focus: "Tehran Yaelekea Kuwa Hatari"
Marekani na Israel wametikisa utaratibu wa Dunia ulioanzishwa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, kwa kuvunja Mamlaka ya Mataifa, kupuuza Diplomasia, na kurejea kwenye hali ya "Sheria ya Msituni".
-
Kiongozi wa Shirika la Awqaf la Iran: Arubaini ya Mwaka Huu Itakuwa na Sura ya Kupinga Uzayuni - Iran ni A'shura ya Dunia ya Leo
Arubaini ya mwaka huu si tu tukio la ibada bali ni ujumbe wa mapambano ya kimaanawi na kisiasa. Iran inachukua nafasi ya kiashura ya dunia, ambapo uongozi, mshikamano, na upinzani dhidi ya dhulma vinaonyeshwa kwa njia halisi.
-
Marekani Yazindua Droni ya LUCAS ikiiga moja kwa moja Droni ya Shahed-136 ya Iran
Fikra hii ya kutengeneza Droni ya LUCAS imetokana na mshangao mkubwa ilioupata Marekani kutoka kwenye Droni Shahid - 136 ya Iran na uwezo wake katika Uwanja wa Kivita, kiasi kwamba Marekani ikaona Iran imepiga hatua kubwa katika masuala ya teknolojia ya Kuzalisha zana za Kivita na za gharama nafuu. Hilo liliifanya Marekani kuwaza kukopi Droni hiyo ya Iran hatimaye kuja na Droni yao waliyoiita LUCAS.
-
Tathmini ya Mashirika 8 ya Kijasusi ya Marekani Kuhusu Kushindwa kwa Trump Katika Kuishambulia Iran
Tathmini nyingi kutoka ndani ya vyombo vya usalama vya Marekani zinaonyesha kuwa Iran bado ina uwezo wa kuendeleza mpango wake wa nyuklia. Badala ya kuuzuia, mashambulizi ya Marekani huenda yameifanya Iran kuwa na msimamo mkali zaidi na kufikiria kuujenga kwa matumizi ya kijeshi.
-
Waduruze - Asili, Itikadi na Ushirikiano wao na Maadui wa Ummah wa Kiislamu (Israel + Marekani)
Katika siku za karibuni, kundi hili limeripotiwa kuhusika katika mauaji ya Waislamu huko Suwayda, Syria, kwa usaidizi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. Waduruze wanajulikana kuwa na uhusiano wa karibu na jeshi la Israel, ambapo vijana wao wengi wanahudumu humo.
-
Balozi wa Iran Nchini Kenya azungumzia: Kukuza Uhusiano wa pande mbili kati ya Iran na Kenya, Umoja wa Kiislamu na Mauaji ya Halaiki Ghaza
Mahojiano hayo yalitoa taswira ya msimamo wa Iran kuhusu masuala ya kimataifa na njia za kuimarisha ushirikiano na nchi za Kiafrika.
-
Uharibifu wa rada ya Kijeshi ya Marekani huko Qatar baada ya Kushambuliwa na Makombora ya Iran
Ulinzi wa anga wa kituo cha Marekani ulifeli Kuzuia Makombora ya Iran, na ajabu ni kwamba Iran ilichagua kuitwanga Kambi hiyo kwa kutumia Makombora ya Zamani.
-
Wayahudi Wanaopinga Uzayuni Wametoa Pongezi kwa Mashahidi wa Mashambulizi ya Israel Dhidi ya Iran
Mayahudi wanao uchukia Uzayuni huko New York, walihudhuria katika Ofisi ya Ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa mjini New York na kutoa heshima zao kwa Mashahidi wa Mashambulizi ya Utawala wa Kizayuni.
-
Mimbari ya Imam Hussein (as) - Nchini Malawi | "Tofauti kati ya Mtu anayemjua Imam Hussein (AS) na Asiyemjua Imam Hussein (as)"
Sheikh Abdul Rahman Kachere: "Mtu anayemfahamu Imam Hussein (AS) daima ni jasiri katika kukabiliana na dhulma".Kumjua vizuri Imam Hussein (as) kutawafanya watu wa mataifa mbalimbali kumpinga adui na dhalimu, na kutambua njama za adui na dhalimu dhidi ya mataifa yao, na kuwa tayari kupambana kwa ajili ya kuinusuru Haki, kwa ajili ya kuondoa uistikbari, dhulma na unyonyaji wa mfumo mpya wa ukoloni unaoitwa: Ukoloni mambo leo.
-
The New York Times: Picha za satelaiti za 2022 zimefichua vituo vitatu vipya vya vifaa vya Kimarekani magharibi mwa Saudi Arabia
Kambi hizi za kijeshi zinaonyesha maandalizi ya mzozo wa muda mrefu na Iran, wakati ambapo Washington inatafuta kuyaweka maeneo katika usalama mbali na Iran ili kuhifadhi vifaa yake vya kijeshi na kupunguza hatari ya kulengwa na kulipuliwa na Iran.