Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Gazeti la Wall Street Journal limeripoti kuwa uwezo wa makombora ya Iran unaweza kuisababishia Marekani na washirika wake hasara za kweli endapo kutazuka mgogoro wa kijeshi katika eneo la Asia Magharibi.
Iran, kwa mujibu wa ripoti hiyo, inategemea hazina kubwa ya silaha yenye mamia ya makombora ya balistiki, ambayo yana uwezo wa kuzingira na kulenga maslahi ya Marekani na washirika wake katika eneo lote la Mashariki ya Kati.
Makadirio yanaonyesha kuwa Tehran inamiliki takribani makombora 2,000 ya balistiki ya masafa ya kati, yanayoweza kufikia maeneo yote ya kikanda, yakiwemo maeneo ya Israel.
Ripoti hiyo pia inabainisha kuwa Iran ina akiba kubwa ya makombora ya cruise ya kuharibu meli, boti za kivita zenye torpedo, pamoja na ndege zisizo na rubani (drones), ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wa meli na manowari za Marekani.
Kwa upande mwingine, Marekani ina mtandao mpana wa vituo vya kijeshi na takribani wanajeshi 40,000 katika eneo hilo, jambo linalofanya ulinzi wa askari na silaha zake kuwa changamoto kubwa katika hali ya mvutano.
Your Comment