Tehran
-
Waziri wa Sayansi wa Iran Aelekea Riyadh Kushiriki Mkutano wa UNESCO Kuhusu Akili Bandia
Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran, Hossein Simaei, ameondoka Tehran kuelekea Riyadh akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu kwa ajili ya kushiriki mkutano wa UNESCO kuhusu akili bandia (AI).
-
Iran na Urusi Zajadili Kuimarisha Ushirikiano Katika Sekta ya Uchapishaji na Vitabu
Iran na Urusi zimejadili njia mpya za kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uchapishaji, ikiwemo kutafsiri na kuchapisha vitabu kwa kubadilishana, kubadilishana haki za uchapishaji, kushiriki katika maonesho ya vitabu na kuandaa miradi ya pamoja ya vitabu vya watoto na vijana.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Iran Haitasalimu Amri Kamwe; Ushindi Dhidi ya Adui katika Vita vya Kiuchumi Unahitaji Jihadi na Kujitolea
Ayatullah Ahmad Khatami amesema Iran haitasalimu amri kamwe, akisisitiza kuwa ushindi dhidi ya vita vya kiuchumi na mashinikizo ya adui unahitaji jihadi, juhudi na kujitolea.
-
Iran na Iraq Zaongeza Ushirikiano katika Masuala ya Kisheria na Kimahakama
Mkuu wa Baraza la Juu la Mahakama nchini Iraq, Jaji Faiq Zidan, amezungumzia na Balozi wa Iraq nchini Iran, Yasser Abdul-Zahra Al-Hajjaj, matokeo ya ziara yake ya hivi karibuni mjini Tehran na juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kimahakama na kisheria kati ya nchi hizo mbili.
-
Mwakilishi wa Hamas Tehran: Uamuzi wa Silaha ni Haki Huru na ya Kimsingi ya Wapalestina
Mwakilishi wa Harakati ya Hamas nchini Iran, Khaled Qadoumi, amesema kuwa uamuzi kuhusu silaha za upinzani ni suala la kitaifa na la mamlaka ya Wapalestina, akisisitiza kuwa hakuna harakati ya upinzani inayoweza kukubali kujinyang’anya silaha wakati mashambulizi dhidi ya Gaza yakiendelea.
-
Iran Yaandaa Mkutano wa 40 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu
Mkutano wa 40 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza leo jijini Tehran, ukishirikisha takribani wageni 600 kutoka ndani na nje ya Iran, wanaowakilisha nchi 40.
-
Iran na Pakistan zakubaliana kuendeleza mashauriano kwa ajili ya amani na usalama wa kikanda
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, na Mkuu wa Jeshi la Pakistan, Field Marshal Asim Munir, wamefanya mazungumzo ya simu na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza mashauriano na juhudi za pamoja kwa ajili ya kuimarisha amani na usalama katika eneo.
-
Mkuu wa Jeshi na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan Waondoka Tehran
Mkuu wa Jeshi na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan wameondoka Tehran Jumatatu jioni, baada ya kumaliza ziara yao ya siku moja. Mazungumzo yao yalihusu kuimarisha ushirikiano wa pande mbili na Iran, pamoja na maendeleo ya kikanda na umuhimu wa kushirikiana katika kukuza amani, utulivu na usalama wa eneo.
-
Kamanda wa Jeshi la Pakistan aelekea Tehran kwa mazungumzo na viongozi wa Iran
Chanzo cha kidiplomasia kimesema Kamanda wa Jeshi la Pakistan, Field Marshal Asim Munir, ameondoka Islamabad kuelekea Tehran kwa ajili ya kukutana na viongozi wakuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
New York Times: Trump arejea kwenye “shinikizo la kiuchumi” dhidi ya Iran baada ya kushindwa kijeshi
Gazeti la New York Times limeripoti kuwa baada ya kushindwa kwa mazungumzo na kupita kwa muda wa mwisho wa siku 60, utawala wa Donald Trump umeelekea tena katika sera ya vikwazo, shinikizo dhidi ya mafuta na vizuizi vya baharini dhidi ya Iran, baada ya kile gazeti hilo linachokiita kutofanikiwa kwa chaguzi za kijeshi.
-
Waziri Mkuu wa Malaysia: Kusimama imara kwa Iran dhidi ya uchokozi kunastahili pongezi
Waziri Mkuu wa Malaysia amelaani uchokozi wa kijeshi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, akisema kuwa msimamo, azma na uvumilivu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na mashambulizi hayo unastahili pongezi.
-
Atlantic: Trump Aelekea Katika Sera ya “Kusubiri na Kuona” Dhidi ya Iran
The Atlantic inaeleza kuwa Trump sasa anaegemea zaidi mkakati wa “kusubiri na kuona”, akitumia shinikizo la kiuchumi na baharini badala ya kuongeza hatua za kijeshi dhidi ya Iran.
-
Waziri wa Mambo ya Ndani Pakistan: Uhusiano Imara wa Tehran na Islamabad Ugeuzwe Kuwa Matokeo ya Kivitendo
Mohsin Naqvi amesema uhusiano wa kina kati ya wananchi wa Iran na Pakistan unapaswa kuzaa ushirikiano zaidi na matokeo ya kivitendo, akisisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi za pamoja katika kufikia malengo ya nchi hizo mbili.
-
Iran na BRICS Zajadili Uanachama wa Tehran katika Benki Mpya ya Maendeleo
Gavana wa Benki Kuu ya Iran, Abdolnaser Hemmati, amekutana na Rais wa Benki Mpya ya Maendeleo ya BRICS, Dilma Rousseff, ambapo pande hizo zimejadili kuendelea kwa mashauriano ya kiufundi kuhusu kujiunga kwa Iran katika benki hiyo na kuimarisha ushirikiano wa kifedha na kifedha-kimataifa.
-
Pakistan: Ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani Tehran Kulenga Kuimarisha Amani na Usalama wa Kikanda
Pakistan imesema ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Mohsin Naqvi, nchini Iran inalenga kuendeleza mashauriano na Tehran kuhusu kuimarisha uhusiano wa pande mbili, ushirikiano wa kiusalama na juhudi za kuimarisha amani na utulivu katika eneo.
-
Moscow na Tehran Zafanya Mashauriano ya Kuimarisha Ushirikiano katika Usalama wa Kimataifa
Iran na Urusi zimefanya mashauriano mjini Moscow kuhusu kuimarisha ushirikiano katika masuala ya usalama wa kimataifa, yakiwemo udhibiti wa silaha, upokonyaji wa silaha na kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia.
-
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan Aelekea Tehran kwa Mazungumzo na Viongozi wa Iran
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan, Seneta Mohsin Raza Naqvi, ameondoka Islamabad kuelekea Tehran kwa ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Mtaalamu wa Marekani: Trump Anajua Mwenyewe Kuwa Iran Haitasalimu Amri
Mchambuzi wa siasa kutoka Chuo Kikuu cha Chicago, Robert Goloty, amesema kuwa hata Donald Trump anatambua kuwa Iran haiwezi kulazimishwa kusalimu amri, na kauli zake kuhusu kujisalimisha kwa Tehran zinaweza kuwa sehemu ya mkakati wa kisiasa wa kupata uungwaji mkono kutoka kwa makundi ya mrengo mkali wa kulia.
-
New York Times: Trump Anakabiliwa na Changamoto ya Kuelewa Viongozi wa Iran
Gazeti la New York Times limesema kuwa Donald Trump ni miongoni mwa marais wa Marekani waliokumbana na ugumu mkubwa wa kuelewa mfumo wa uongozi wa Iran, hali iliyochangia kuongezeka kwa msuguano kati ya Washington na Tehran.
-
Financial Times: Trump Akwama Kati ya Kuongeza Vita na Iran au Kukubali Makubaliano
Gazeti la Financial Times linaripoti kuwa Rais wa Marekani Donald Trump anakabiliwa na chaguo gumu kati ya kuongeza mzozo na Iran au kukubali makubaliano yanayozingatia masharti ya Tehran, hali inayoonyesha kupungua kwa nafasi za Washington katika sera yake dhidi ya Iran.
-
Watafiti waalikwa kuwasilisha tafiti katika Kongamano la Pili la Kimataifa la Ustaarabu wa Kiirani na Kiislamu litakalofanyika Vienna
Kongamano la Pili la Kimataifa la Ustaarabu wa Kiirani na Kiislamu limetoa wito kwa wasomi, watafiti na wanafunzi wa shahada za juu kutoka duniani kote kuwasilisha tafiti zao, huku mada kuu ikiwa ni nafasi ya wanawake katika ustaarabu wa Kiirani tangu zama za kale hadi leo.
-
Mhadhiri wa Sala ya Ijumaa Tehran: Makombora na Diplomasia Vimeimarisha Mizani ya Nguvu kwa Manufaa ya Iran
Mhadhiri / Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema uwezo wa makombora ya Iran pamoja na diplomasia madhubuti ndivyo vilivyoimarisha mizani ya nguvu kwa manufaa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, huku akisisitiza umuhimu wa kulinda mshikamano wa kitaifa na kuimarisha imani ya wananchi.
-
Iran na China zalaani mashambulizi dhidi ya miundombinu muhimu ya Iran na uhalifu wa kivita
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, na mwenzake wa China, Wang Yi, wamejadili uhusiano wa kimkakati kati ya Tehran na Beijing, huku wakilaani mashambulizi dhidi ya miundombinu muhimu ya Iran na uhalifu wa kivita, pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha amani na utulivu katika Asia Magharibi.
-
Khatibu wa Ijumaa Tehran: Imam Shahidi alivunja nguvu za ubeberu wa kimataifa
Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa Imam Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei (r.a.) alichagua njia ya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na, kupitia mapambano yake kabla na baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, aliweza kuvunja nguvu za ubeberu wa kimataifa.
-
Iran Yalaani Vikali Shambulio la Kigaidi Kusini Magharibi mwa Pakistan
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baqaei, amelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea katika mji wa Khuzdar kusini magharibi mwa Pakistan, akitoa salamu za pole kwa familia za wahanga na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikanda katika kupambana na ugaidi.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Akutana na Mwenzake wa Kazakhstan Kujadili Uhusiano wa Nchi Mbili
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Araghchi, amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kazakhstan, Yermek Kosherbayev, ambapo viongozi hao wamejadili kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.
-
Hali ya Majonzi Yatanda Tehran sambamba na kuanza kwa Shughuli za Kumuaga Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Hali ya majonzi na huzuni kubwa imeendelea kutawala katika mji wa Tehran kuelekea shughuli za mwisho za kumuaga Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei(Ra), huku umma wa Kiislamu ukiendelea kutoa heshima zake kwa Kiongozi huyu Mwema na mtetezi wa Haki za Wapalestina na Haki za wanyonge popote walipo Ulimwenguni.
-
Mamia ya Waandishi wa Habari wa Kimataifa Kuutangaza Msiba wa Mazishi ya Kiongozi Shahidi Tehran
Mkuu wa Mkoa wa Tehran ametangaza kuwa kati ya waandishi wa habari 500 hadi 600 wa kimataifa wanatarajiwa kushiriki katika kuripoti hafla ya mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, sambamba na maandalizi makubwa ya kiafya na kiusalama kwa ajili ya kuhudumia umati mkubwa wa waombolezaji.
-
Iran: Mashambulizi ya Marekani Kusini mwa Nchi Yathibitisha Kutoheshimu Ahadi za Kimataifa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya vituo vya ufuatiliaji kusini mwa Iran, ikisema kuwa hatua hiyo inaonesha wazi kwamba Washington haithamini wala kuheshimu ahadi na wajibu wake wa kimataifa.
-
Pakistan: Ziara ya Rais Pezeshkian Islamabad Yaakisi Dhamira ya Pamoja ya Amani na Maendeleo ya Kikanda
Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan imesema ziara rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, nchini Pakistan inaonesha azma ya pamoja ya Tehran na Islamabad ya kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kitamaduni, pamoja na kuendeleza amani, utulivu na maendeleo endelevu katika eneo.