17 Juni 2025 - 21:27
Onyo la Jeshi la Iran kwa Walowezi wa Israel | Ondokeni katika Maeneo yote ya Israel haraka ili muokoe Nafsi zenu

Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran linajiandaa na shambulizi kubwa ambalo wameliita kuwa litakuwa ni shambulizi la Kutoa adhabu kwa Adui Israel. Kutokana na hilo imewataka Walowezi wa Kizayuni kutoka ndani ya Israel haraka Sana ili waokoe Nafsi zao.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -Abna- Kiongozi wa Majeshi ya Iran ametoa onyo kali kwa walowezi Waisraeli walio katika maeneo ya Tel-Aviv na Haifa na maeneo mengine ya Palestina yanayokaliwa kimabavu na Utawala haram wa Kizayuni, na kuwataka waondoke mara moja katika mane yote, huku Iran ikijiandaa kutekeleza mashambulizi makubwa ambayo imeyaita yatakuwa ni Mashambulizi ya kutoa adhabu, yanayotarajiwa kuenea katika ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu na Utawala huo Ghasibu wa Israel.

Taarifa hiyo imetolewa na Jenerali Mousawi, Mkuu wa Vikosi vya Kijeshi vya Iran, akisisitiza kuwa Walowezi hao wanatakiwa kutoka Haraka katika maeneo yote ya Israel kabla ya Mashambulizi Makali kuanza. 

Pia, taarifa hiyo imeongeza kuwa Iran inajipanga 'kulipiza kisasi kikali' kufuatia uchokozi wa kijeshi wa hivi karibuni kutoka Israel na inakemea utawala wa waziri mkuu Netanyahu akieleza kuwa umekata tamaa, umejaa ufisadi, na ni wa kihalifu,' akisema kuwa uchokozi wao wa hivi karibuni wa kijeshi 'utaibua maangamizi'. Ametoa onyo kuwa majibu ya Iran yatalenga maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu.

Aidha, ameendelea kueleza kuwa jeshi la Iran lina 'idadi kubwa ya taarifa za kijasusi' kuhusu maeneo nyeti  katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel, huku akiwaonya walowezi kuepuka maeneo hayo na kubainisha kuwa hata maficho ya chini ya ardhi hayatadhamini usalama wao.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha