Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema: Tutajibu ongezeko la mvutano kwa ongezeko la mvutano. Kuanzia sasa, sambamba na kupiga marufuku kupita kwa meli za Israeli katika Bahari Nyekundu, kupita kwa meli za Marekani pia ni marufuku.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Washington haina haki ya kulazimisha siasa za nje za Iran, na kuitaka kusimamisha mara moja mauaji yake kwa watu wa Yemen.