1 Desemba 2025 - 21:03
“Barna”, mgombea madhubuti wa kuchukua nafasi ya Benjamin Netanyahu

Kwa mujibu wa madai ya tovuti moja ya Kizayuni, vyanzo vya kisiasa nchini Israel vinamtaja David Barna, mkuu wa Mossad, kama mmoja wa wagombea wakuu wa kumrithi Benjamin Netanyahu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- hatua ya hivi karibuni ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, ya kuwasilisha ombi la msamaha siku ya Jumapili, imeibua mgawanyiko mkubwa katika mtazamo wa umma wa Israel.
Wapinzani wa Netanyahu, wakisisitiza juu ya ulazima wa “kukiri hatia” na kuondoka kabisa katika uwanja wa siasa, wamepinga ombi hilo.

Katika mazingira haya, baadhi ya vyanzo vya Kizayuni vinaanza kutoa tetesi kuhusu watu wanaoweza kumrithi Netanyahu.

Tovuti ya habari Israel National News imedai kuwa vyanzo vya kisiasa nchini Israel vinamtaja David Barna, mkuu wa Mossad, kama mmoja wa wagombea wakuu wa kuchukua nafasi ya Benjamin Netanyahu.

Uwezo wa Barna katika kusimamia operesheni za kijasusi na kuongeza nafasi ya Mossad katika mabadiliko ya eneo umeimarisha nafasi yake katika medani ya siasa za Israel.

Anayasema wachambuzi wa Israel ni kwamba, endapo Israel itaingia katika hatua mpya ya kukabiliana na Iran, Barna anaweza kuwa miongoni mwa sura muhimu zaidi katika mustakabali wa siasa za nchi hiyo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha