vyanzo
-
Pakistan: Marekani na Iran Ziko Karibu Kufikia Makubaliano ya Amani — Bloomberg
Pakistan imesema Marekani na Iran ziko karibu kufikia makubaliano mapya kuhusu amani, huku Islamabad ikiendelea na juhudi za upatanishi kati ya Washington na Tehran tangu kuanza kwa mzozo.
-
Yemen: Maafisa wa Saudi Arabia Wauawa na Kujeruhiwa katika Mashambulizi ya Vikosi vya Yemen Mjini Al-Mokha
Vyanzo vya Al-Masirah vimeripoti kuwa maafisa kadhaa wa Saudi Arabia wameuawa na wengine kujeruhiwa katika operesheni ya hivi karibuni iliyolenga mikusanyiko ya vikosi vya Saudi Arabia katika eneo la Al-Mokha, huku milipuko na nguzo za moshi zikiendelea kuonekana katika maghala ya silaha yaliyoko katika pwani ya magharibi mwa Yemen.
-
IRGC yadai kulenga Kambi ya Anga ya Amir Hassan nchini Jordan kwa makombora na ndege zisizo na rubani
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), vikosi vyake vimedai kulenga majukwaa ya makombora, maghala ya mafuta na maeneo ya kuhifadhia silaha katika Kambi ya Anga ya Amir Hassan nchini Jordan, katika kile ilichokieleza kuwa ni hatua ya kujibu ukiukaji uliofanywa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Mzozo wa Urani Wazidi Kutatiza Makubaliano Kati ya Iran na Marekani
Ripoti zinaeleza kuwa Iran inaendelea kusimama kidete katika msimamo wake wa kutoruhusu akiba yake ya urani iliyorutubishwa kuhamishwa nje ya nchi, jambo linaloongeza ugumu katika mazungumzo yanayoendelea na Marekani kuhusu makubaliano mapya ya nyuklia na usalama wa kikanda.
-
Mashahidi katika shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya Msikiti wa Mashia katika mji mkuu wa Pakistan
Mashahidi 31 katika shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya msikiti wa Mashia katika mji mkuu wa Pakistan Kufuatia shambulio la kujitoa mhanga katika moja ya misikiti ya Mashia huko Islamabad, angalau watu 31 wamepata shahada.
-
Kukamatwa kwa mtuhumiwa wa kushiriki katika mauaji ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah
Mwandishi wa habari wa Lebanon ametangaza kuwa mtu aliyeko chini ya ulinzi wa Idara ya Usalama wa Umma ya Lebanon alihusika kwa kushirikiana na Israel na kukusanya taarifa zilizopelekea kuuawa kwa Sayyid Hassan Nasrallah.
-
Kiongozi wa Iran Afichua Malengo ya Marekani Juu ya Utajiri wa Taifa la Iran
Imam Khamenei amesema Iran inalengwa na Marekani kutokana na utajiri wake wa asili na nafasi yake ya kijiografia, akibainisha kuwa mafuta, gesi na madini ya thamani ni miongoni mwa vivutio vinavyoifanya Iran kuwa shabaha ya tamaa ya kibeberu. Kauli hiyo aliitoa wakati wa maadhimisho ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Taliban Wamefunga Kituo cha Kielimu na Kitamaduni cha Imam Hussein (a.s) Jijini Kabul
Kituo cha Kielimu na Kitamaduni cha Imam Hussein (a.s) kilihesabiwa kuwa miongoni mwa vituo hai vya kitamaduni vya Waislamu wa Kishia katika magharibi mwa Kabul. Kufungwa kwake kumeibua hisia na malalamiko miongoni mwa wakazi wa eneo hilo na wanaharakati wa kitamaduni, ambao wameeleza wasiwasi wao kuhusu mustakabali wa shughuli za kielimu na kitamaduni za jamii hiyo chini ya utawala wa sasa.
-
“Barna”, mgombea madhubuti wa kuchukua nafasi ya Benjamin Netanyahu
Kwa mujibu wa madai ya tovuti moja ya Kizayuni, vyanzo vya kisiasa nchini Israel vinamtaja David Barna, mkuu wa Mossad, kama mmoja wa wagombea wakuu wa kumrithi Benjamin Netanyahu.
-
Ushahidi wa Kifo cha Kishahidi cha Bibi Fatimah az-Zahra (a.s) | Mtizamo wa Shia na Sunni juu ya Kifo Hicho
Ushahidi wa Riwaya za Kisunni: Shia pia wametaja kuwa baadhi ya maelezo kuhusu tukio la shambulio la nyumba ya Bibi Fatimah (a.s.) na Imam Ali (a.s.) yanapatikana hata katika baadhi ya vitabu vya Kisunni, na wamekusanya riwaya zaidi ya 84 kutoka kwa wanazuoni wa Kisunni kuhusu tukio hilo (kama ilivyokusanywa katika al-Hujūm ʿalā Bayt Fāṭimah (a.s).
-
Netanyahu: Uwepo wa Uturuki Gaza ni mstari mwekundu kwa Israel
Vyombo vya habari vya Israeli vimereport kuwa Binyamin Netanyahu amekataa kabisa hatua yoyote ya Uturuki kushiriki katika Ardhi ya Ukanda wa Gaza.