Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Polisi wa mji mkuu wa Pakistan walitangaza kuwa kufuatia shambulio la kujitoa mhanga lililolenga moja ya misikiti ya Mashia katika mji wa Islamabad, angalau watu 31 wameuawa na wengine 169 kujeruhiwa. Takwimu hizi ni za awali, na shambulio hilo lilitokea wakati wa Sala ya Ijumaa huku kukiwa na idadi kubwa ya waumini.
Vyanzo vya Polisi wa Pakistan vilitabiri kuwa idadi ya waathirika huenda ikaongezeka.
Vyanzo vya kiusalama vya Pakistan vilitangaza kuwa “mshambuliaji wa kujitoa mhanga” alipositishwa katika mlango wa msikiti wa Mashia uliopo katika eneo la Tirlai pembezoni mwa Islamabad, alijilipua mwenyewe.

“Shahbaz Sharif,” Waziri Mkuu wa Pakistan, alilaani shambulio hilo na akataka wahusika wafuatiliwe na waadhibiwe.
Picha zilizosambazwa kutoka eneo la mlipuko zinaonyesha miili iliyolowa damu ikiwa imelala sakafuni mwa msikiti na miongoni mwa vioo vilivyopasuka na vifusi, huku hali ya hofu na mshangao ikiwatawala waumini.
Makumi ya majeruhi wengine pia walikuwa wameanguka katika uwanja na bustani ya nje ya Msikiti, na watu walikuwa wakipiga kelele kuomba msaada.
Kutokea kwa mlipuko katika mji mkuu wa Pakistan ambao uko chini ya ulinzi mkali wa kiusalama ni jambo nadra, hata hivyo Pakistan katika miaka ya hivi karibuni imeshuhudia kuongezeka kwa wimbi la vurugu.

Your Comment