Wanafunzi 144 wa Hawzah ya Wasichana ya Hazrat Zainab (s.a) pamoja na wasimamizi wao huanza kila siku yao kwa kusoma Qur’an Tukufu na dua, katika juhudi za kuhuisha nafasi ya Qur’an na Dua katika maisha ya kila siku ya Muislamu.

20 Julai 2026 - 15:05

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s.) –ABNA– Wanafunzi 144 wa Shule ya Wasichana ya Hazrat Zainab (s.a), iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam, Tanzania, kila Siku huuisha utamaduni maalumu wa Kiislamu wa kuanza siku yao kwa kusoma Qur’an Tukufu na Dua.

Hatua hii ni yenye lengo la kuhuisha utamaduni wa Kiislamu wa kuifanya Qur’an Tukufu na Dua kuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ya Muislamu.

Katika mpango huo, wanafunzi hao pamoja na wasimamizi wao hushiriki katika ibada (Sala) ya Asubuhi inayoambatana na usomaji wa Qur’an na Dua, huku wakisisitiza umuhimu wa kumweka Mwenyezi Mungu na Kitabu Chake Kitukufu mbele ya mambo yote katika maisha.

Shule ya Wasichana ya Hazrat Zainab (s.a) inaeleza kuwa kuanza siku kwa Qur’an na Dua ni hatua muhimu katika kumjenga Muislamu mwenye uhusiano wa karibu na Qur’an Tukufu, dua na maadili ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa mpango huo, Qur’an haipaswi kuwa kitabu kinachosomwa katika nyakati maalumu pekee, bali inapaswa kuwa mwongozo wa maisha ya Muislamu na kupewa nafasi ya kwanza katika mwenendo wa kila siku.

Maoni yako

You are replying to: .
captcha