Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Netanyahu anapinga kushiriki kwa Uturuki katika Gaza, ama kupitia vikosi vya kimataifa kuleta utulivu au kupitia makampuni ya ujenzi kwa ajili ya urejeshaji wa hali nzuri na tulivu ya Gaza.
Gazeti la Maariv liliandika kuwa katika mkutano wake na Steve Witkoff na Jared Kushner, wajumbe wa Rais wa Marekani, Netanyahu alituma ujumbe mkali akisema:
"Hatutaruhusu Uturuki kuwepo Gaza."
Vyanzo vya kisiasa vimeripoti kuwa Netanyahu katika siku za hivi karibuni amewasilisha ujumbe thabiti kwa serikali ya Marekani na washauri wake wa ngazi ya juu, akisisitiza kuwa Israel inapingana vikali na ushiriki wa Uturuki katika kikosi cha kimataifa kitakachoingia Gaza baada ya kufikiwa kwa mapumziko ya mapigano.
Netanyahu alibainisha kuwa:
"Uwepo wa Uturuki Gaza - iwe kijeshi, kiusalama au kisio rasmi - ni mstari mwekundu kwa Israel" na kuongeza kuwa anaihisi Uturuki kama mwenye hasira katika eneo na hakuna nafasi katika mpango wa kimataifa wa kuweka utulivu Gaza.
Aidha, alirejelea kauli za wazi za Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, dhidi ya Israel na uhusiano wa Ankara na Hamas, akasema:
"Israel haitakubali uhalali wa uwepo wa Uturuki Gaza chini ya jina la misaada ya kibinadamu au urejeshaji usio wa kijeshi."
Your Comment