7 Desemba 2025 - 16:41
Ushindi wa Jukwaa la Upinzani (Muqawama) ni Kudhihirika kwa Utabiri wa Qur’an

Kushindwa kwa Israel na Marekani katika mapambano ya hivi karibuni kunatokana na uongozi wa busara wa Ayatullah Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- QumIran | Hujjatul-Islam wal-Muslimin Khamoushi, katika hafla ya kufunga mashindano ya Qur’ani Tukufu iliyofanyika katika mji wa Qum, Iran, amewapongeza Waislamu kwa maadhimisho ya kuzaliwa kwa Bibi Sayyida Fatima Zahra (a.s), na kuchambua matukio ya hivi karibuni katika eneo la Mashariki ya Kati kwa kuzingatia mafundisho ya Qur’ani Tukufu.

Amesema kuwa kushindwa kwa Israel na Marekani katika mapambano ya hivi karibuni kunatokana na uongozi wa busara wa Ayatullah Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Amesisitiza kuwa mapambano haya yanaendana kikamilifu na utabiri wa Qur’ani Tukufu, hususan katika Suratul Hashr, ambapo tabia za wanafiki wa wakati ule zinafanana na tabia za wanafiki na watawala wanaotafuta kurejesha utawala wa kifalme katika zama hizi, ambao waliwaahidi maadui ushindi wa uongo.

Hofu Kubwa ya Adui Dhidi ya Iran

Mwenyekiti wa Shirika la Wakfu (Awqaf), kwa kunukuu Aya za Qur’ani, alibainisha kuwa maadui wana hofu kubwa dhidi ya taifa la Iran, na akauliza kwa nini watu kama Donald Trump bado wanaendelea kulitaja jina la Shahidi Qasem Soleimani, jambo ambalo, kwa mujibu wake, linaonyesha nguvu kubwa ya ushawishi wa upinzani katika uwanja wa kimataifa.

Uchamungu wa Kijamii na Ramani ya Hatua ya Pili ya Mapinduzi

Hujjatul-Islam Khamoushi alieleza kuwa maana ya msingi ya taqwa (uchamungu) katika medani hii ni uchamungu wa kijamii, na akasisitiza umuhimu wa kuifuata ramani ya njia iliyoainishwa na Kiongozi wa Mapinduzi katika Tamko la Hatua ya Pili ya Mapinduzi ya Kiislamu (Bayānīyeh-e Gām-e Dovvom-e Enqelāb).

Ushindi wa Yemen ni Matunda ya Mafundisho ya Qur’an Tukufu

Amehitimisha kwa kusema kuwa mafanikio ya Jukwaa la Upinzani, yakiwemo msimamo thabiti wa Yemen dhidi ya Marekani, yametokana na kufuata kwa dhati mafundisho ya Qur’ani na utiifu kamili kwa Kiongozi wa Umma (Waliyyul-Amr).

Pia ameonyesha matumaini yake kuwa kuimarika kwa uelewa wa kina wa Qur’ani Tukufu kutakuwa ni utangulizi wa kutimia kwa malengo makubwa zaidi na kutaandaa mazingira ya kuja kwa Imam Mahdi (a.j), na kwamba Iran itaweza kusimama imara na kushinda katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijeshi na kisiasa dhidi ya mfumo wa ubeberu wa kimataifa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha