Qur’an Tukufu
-
Kumbukumbu ya Shahada ya Imam Hasan al-Askari (AS)
Mojawapo ya malengo ya Mitume na Maimam (amani iwe juu yao), ni kusimamisha uadilifu na usawa katika jamii. Kwa mujibu wa Qur'an na hadithi za Maimamu, jamii haiwezi kusimama bila ya uongozi wa Imam Mwadilifu atakayeongoza masuala ya kidini na kijamii. Imam ni mlinzi wa sheria na mwongoza watu kuelekea haki na mafanikio.
-
(Muqawamah) Kusimama dhidi ya Ubeberu ni Fahari ya Mataifa ya Waumini
"Kazi yetu kuu ni kuinua bendera ya Qur’an ili kwa kueneza mtindo sahihi wa maisha, jamii ya Kiqur’ani iweze kuundwa. Ikiwa nchi za Kiislamu zitaifuata Qur’an, zitauweza kuwalazimisha maadui kurudi nyuma"
-
Mahojiano Maalum ya Firdaus TV na Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum - Mwenyekiti JMAT-TAIFA Yaliyofanyika Katika Uwanja wa Michezo wa Mkwakwani, Tanga
Ni katika Kongamano la Qur'an Tukufu lililofanyiks Jijini Tanga. Tukio hilo liliimarisha misingi ya Amani, Mshikamano, Maridhiano, na Ushirikiano kati ya Watanzania, likiwa ni Jukwaa la kuendeleza Mafundisho ya Qur’an Tukufu yanayohimiza Utulivu na Maelewano ya Kijamii.
-
Mkutano wa kihistoria wa Marjaa wa Kidini:
Najaf Ashraf: Ayatollah Jawadi Amuli akutana na Ayatollah Sistani / Zawadi ya Qur'an yatolewa katika Mkutano wa Viongozi hawa wawili wa juu wa Kidini
"Ayatollah al-Udhma Jawadi Amuli — ambaye yuko ziarani nchini Iraq kwa ajili ya kutembelea maeneo matakatifu — amekutana na kufanya mazungumzo na Ayatollah al-Udhma Sistani huko Najaf Al-Ashraf."
-
Jinsi ya kuthibitisha Isma ya Maimamu 9 (a.s) kutoka ndani ya Qur’an Tukufu
“Na (Kumbukeni) Ibrahim alipojaribiwa na Mola wake kwa matamko, naye akayatimiza. Akasema: Hakika mimi nitakufanya kuwa Imam wa watu. Ibrahim akasema: Je,na Kizazi changu (pia)?.(Ndiyo, lakini) ahadi yangu haiwafikii Madhalimu.”