4 Desemba 2025 - 22:09
Ustadhi Rajai Ayoub na Wasomi wa Qur'an kutoka Tanzania Wawasili Salama Bangladesh kwa Ajili ya Mahfali Makubwa ya Kimataifa ya Qur'an +Picha

Mahfali hayo ya kimataifa yanakusudiwa kuwa jukwaa muhimu la kiroho na kielimu, ambapo wasomaji bingwa na mahiri wa Qur'an Tukufu kutoka Tanzania watapata fursa ya kuonesha vipaji vyao katika kusoma Aya Tukufu za Mwenyezi Mungu (SWT), kwa mapito na mitindo mbalimbali ya usomaji wa Qur'an (Qira’at).

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ustadhi Rajai Ayoub pamoja na wasomi wenzake wa Qur'an Tukufu kutoka nchini Tanzania wamewasili salama nchini Bangladesh na kupokelewa kwa mapokezi mazuri yaliyojaa upendo, heshima na ukarimu mkubwa kutoka kwa Waislamu wa nchi hiyo.

Ustadhi Rajai Ayoub na Wasomi wa Qur'an kutoka Tanzania Wawasili Salama Bangladesh kwa Ajili ya Mahfali Makubwa ya Kimataifa ya Qur'an +Picha

Kwa mujibu wa ratiba yao, leo tarehe 4 Disemba, 2025, wanatarajiwa kushiriki katika Mahfali Makubwa ya Kimataifa ya Usomaji wa Qur'an Tukufu, tukio tukufu linalotarajiwa kuhudhuriwa na wapenzi wengi wa Qur'an kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Bangladesh.

Mahfali hayo ya kimataifa yanakusudiwa kuwa jukwaa muhimu la kiroho na kielimu, ambapo wasomaji bingwa na mahiri wa Qur'an Tukufu kutoka Tanzania watapata fursa ya kuonesha vipaji vyao katika kusoma Aya Tukufu za Mwenyezi Mungu (SWT), kwa mapito na mitindo mbalimbali ya usomaji wa Qur'an (Qira’at).

Tukio hili kubwa linaonyesha nafasi adhimu ya Tanzania katika kuendeleza elimu ya Qur'an na kuwatangaza wasomaji wake katika ngazi ya kimataifa. Pia ni ishara ya udugu wa Kiislamu unaounganisha mataifa ya Kiislamu katika upendo wa Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (SWT) awawekee wepesi katika shughuli hii tukufu, awalinde katika safari na katika hafla yote, na Insha’Allah waiwakilishe vyema Tanzania katika usomaji wa Aya Tukufu za Qur'an. Aidha, tunamuomba Allah awape tawfiq ya kueneza nuru ya Qur'an kwa wapenzi wote watakaohudhuria mahfali hayo.

Ustadhi Rajai Ayoub na Wasomi wa Qur'an kutoka Tanzania Wawasili Salama Bangladesh kwa Ajili ya Mahfali Makubwa ya Kimataifa ya Qur'an +Picha

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha