2 Desemba 2025 - 15:43
Marafiki wa Ukweli Wako Wengi Zaidi Upande wa Pili | Kifo cha Kishahidi kwao hakileti upweke kwao Bali ni Daraja la kukutana na Msafara wa Waumini

"Katika ugeni hakuna hofu ya upweke; marafiki wapendwa wako wengi zaidi upande ule mwingine.” Kwa maana kwamba: Shahidi anapovuka kutoka dunia hii, haogopi kutengwa, kwa sababu anatambua wazi kuwa upande wa pili kuna kundi kubwa la wacha-Mungu, wakweli, watu wema, na mashahidi waliomtangulia, walio tayari kumpokea katika safu yao.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mashahidi wa Uislamu halisi hawapati upweke katika safari yao ya haki; hata pale wanapokuwa mbali, katika ugeni, au katika mazingira magumu yanayoonekana kana kwamba hayana msaada. Ugeni kwao si mwisho wa njia, bali ni mwanzo wa kuungana kwa kina na msafara wa watu wa haki waliotangulia, Mitume, Manabii, Maswali na Waumini vipenzi wa Mwenyezi Mungu.

Kwa shahidi, kifo si kukatika au kuachwa peke yake - bali ni daraja la kuungana tena na marafiki wa Mwenyezi Mungu; wale waliopita katika njia ya nuru na sasa wanasubiri kwa matarajio huko upande wa pili.

Ndiyo maana inasemwa:
“Katika ugeni hakuna hofu ya upweke; marafiki wapendwa wako wengi zaidi upande ule mwingine.”

Shahidi anapovuka kutoka dunia hii, haogopi kutengwa, kwa sababu anatambua wazi kuwa upande wa pili kuna kundi kubwa la wacha-Mungu, wakweli, watu wema, na mashahidi waliomtangulia, walio tayari kumpokea katika safu yao.

Ugeni wa dunia kwa shahidi ni lango la muungano-muungano na haki, muungano na Mola, na muungano na ule mkondo uleule uliotembelewa na Mitume, Mawalii, na mashahidi wa karne zote.

Huu ndiyo ujumbe unaobaki kwa kila anayetembea katika njia ya msimamo na uadilifu:
Njia ya haki, ingawa ni ngumu, haijawahi kuwa ya upweke; na upande wa pili wa majaribu, kuna uunganisho mpana zaidi unaongoja.

Marafiki wa Ukweli Wako Wengi Zaidi Upande wa Pili | Kifo cha Kishahidi kwao hakileti upweke kwao Bali ni Daraja la kukutana na Msafara wa Waumini

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha