"Katika ugeni hakuna hofu ya upweke; marafiki wapendwa wako wengi zaidi upande ule mwingine.”
Kwa maana kwamba: Shahidi anapovuka kutoka dunia hii, haogopi kutengwa, kwa sababu anatambua wazi kuwa upande wa pili kuna kundi kubwa la wacha-Mungu, wakweli, watu wema, na mashahidi waliomtangulia, walio tayari kumpokea katika safu yao.
Ali (a.s), wapo Watu waliodai kuwa wanampenda, mpaka wakamfanya kuwa ni mungu, ametakasika Mwenyezi Mungu na wanayo mshirikisha nayo. Na wapo watu waliomchukia na wakampiga vita, wakamtukana na kumlaani, wakakufuru na wakatoka katika Uislamu. Na wapo baadhi ya Watu waliompenda, wakawa watiifu kwake, na wakashikamana naye kama alivyoamrisha Mtume (s.a.w.w), basi kwa hakika hao ndio waumini wa kweli.