18 Machi 2025 - 14:35
Ushahidi wa Mawalii Katika Kumfananisha Ali na Manabii

Ali (a.s), wapo Watu waliodai kuwa wanampenda, mpaka wakamfanya kuwa ni mungu, ametakasika Mwenyezi Mungu na wanayo mshirikisha nayo. Na wapo watu waliomchukia na wakampiga vita, wakamtukana na kumlaani, wakakufuru na wakatoka katika Uislamu. Na wapo baadhi ya Watu waliompenda, wakawa watiifu kwake, na wakashikamana naye kama alivyoamrisha Mtume (s.a.w.w), basi kwa hakika hao ndio waumini wa kweli.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Mtume Muhammad (s.a.w.w) alimwambia Imam Ali (A.S):

《فيكَ مثلٌ مِنْ عيسى أبغضَتْه اليهودُ حتى بَهَتوا أمَّه وأحبَّتْه النصارى حتى أنزلوه بالمنزلةِ التي ليستْ بهِ

ثم قال علي ع :《 يَهلَكُ فيَّ رجلان محبٌّ مُفرِطٌ يُقرِّظُني بما ليس فيَّ ومُبغضٌ يحملُه شَنَآني على أن يَبْهتني》

《مسند أحمد ٣٥٥/٢ قال احمد شاكر: إسناده حسن》

Utakuwa na kisa kama cha Isa (a.s): Mayahudi walimfanyia Uadui mpaka wakamkashifu Mama yake, na Wakristo walimpenda sana mpaka wakampandisha cheo asichostahili (wakamuita mwana wa Mungu au mungu wao!).

Kisha Imam Ali (amani iwe juu yake) akasema:
"Kuhusu mimi, watu wawili wameharibikiwa na wataangamizwa: Mwenye kunipenda mpaka kuvuka mipaka, ambaye ananisifu kwa sifa nisiyostahili, na adui mwenye kunichukia, ambaye uadui wake kwangu unamlazimisha kunikashfu" / Rejea: Musnad Ahmad: Juzuu ya 2. Ukurasa wa 355. Ahmad Shakir amesema: Silsila (Sanad) yake ni Hasan.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema ndani ya Qur'an Tukufu: 

قال تعالى:《إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ اللَّهِ كَمَثَلِ آدَمَ ۖ خَلَقَهُ مِن تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُن فَيَكُونُ}

《آل عمران ٥٩》

"Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu, ni kama mfano wa Adam; alimuumba kutokana na udongo, kisha akamwambia 'kuwa', akawa"

《Surat Aali Imran: Aya ya 59》

Je, ni Fadhila ipi hii kwa Amirul-Muuminin (a.s), kiasi kwamba mpaka Mtume (s.a.w.w) akamfananisha na Isa bin Maryam (a.s)?!.

Na tunasema:

عليٌ ع ادّعى قوم حبه فجعلوه إلها، تعالى الله عما يشركون. وأبغضه قومٌ فحاربوه وسبّوه ولعنوه، فكفروا وخرجوا من الإسلام. وأحبّه قوم فأطاعوه ووالوه وتمسّكوا به كما أمر النبي، فأولئك هم المؤمنون حقا

Ushahidi wa Mawalii Katika Kumfananisha Ali na Manabii

Ali (a.s), wapo Watu waliodai kuwa wanampenda, mpaka wakamfanya kuwa ni mungu, ametakasika Mwenyezi Mungu na wanayo mshirikisha nayo. Na wapo watu waliomchukia na wakampiga vita, wakamtukana na kumlaani, wakakufuru na wakatoka katika Uislamu. Na wapo baadhi ya Watu waliompenda, wakawa watiifu kwake, na wakashikamana naye kama alivyoamrisha Mtume (s.a.w.w), basi kwa hakika hao ndio waumini wa kweli.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha