Wito wa kuimarisha hekima, uadilifu na umoja ndani ya Umma wa Kiislamu umetolewa, ukisisitiza kuwa tofauti za kimtazamo na kimadhehebu hazipaswi kuwa chanzo cha chuki bali fursa ya majadiliano ya kielimu na kuheshimiana.
Sikukuu ya Ghadir, ambayo ni miongoni mwa sikukuu kubwa zaidi kwa Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashari, ambapo huadhimisha ndani yake kutangazwa kwa wilayat ya Imam Ali ibn Abi Talib(as). Katika siku hii, Waumini huhimizwa kufanya amali mbalimbali za ibada na kheri kama vile kuswali, kusoma dua, kutoa sadaka na kuwalisha wengine, huku wakitumia fursa hiyo kuimarisha maarifa ya dini, kuhuisha ahadi yao katika kushikamana na Ahlul-Bayt (a.s) na kuimarisha mshikamano wa kijamii na kiroho.
Tarehe 13 ya mwezi wa Rajab ni siku ya kuzaliwa kwa Imam Ali (a.s), kiongozi mkuu baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambaye ni mtu pekee aliyezaliwa ndani ya Al-Kaaba Tukufu na anayetambuliwa kwa elimu, uadilifu, ujasiri na maadili mema kwa wanadamu wote.