Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Tarehe 13 ya mwezi mtukufu wa Rajab ni siku adhimu katika historia ya Uislamu, kwani ndiyo siku aliyozaliwa kiongozi mkubwa baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), Sayyidina Ali ibn Abi Talib (a.s).
Imam Ali (a.s) ni mtu pekee katika historia ya binadamu aliyezaliwa ndani ya Al-Kaaba Tukufu, kibla cha Waislamu wote duniani, tukio linaloashiria daraja yake ya kipekee mbele ya Mwenyezi Mungu na nafasi yake tukufu katika Uislamu.
Sayyidina Ali (a.s) pia ndiye mtu wa pekee aliyeruhusiwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) kumuoa binti yake mpendwa, Sayyida Fatima Zahra (a.s), ndoa iliyobarikiwa na kuzaa kizazi kitukufu cha Imam Hasan (a.s), Imam Husayn (a.s) na Sayyida Zaynab (a.s), ambao walibeba na kuendeleza ujumbe wa haki, subira na kujitolea katika Uislamu.
Imam Ali (a.s) anakumbukwa kwa sifa nyingi tukufu, zikiwemo elimu yake pana, ushujaa wake usio na kifani, ukarimu, uadilifu, na maadili mema kwa watu wote, bila kujali dini, kabila au asili yao.
Maisha yake yanabaki kuwa kielelezo cha uongozi wa haki, kupigania ukweli na kuwatumikia wanyonge, na mafundisho yake yanaendelea kuwa mwanga kwa wanadamu hadi leo.
Je, wewe unamtambua Imam Ali (a.s) kama nani katika maisha yako?.
Your Comment