Sherehe hiyo ya Mazazi ya Mtume wa Ummah (saww), imeonesha mshikamano, mapenzi ya dhati, na hamasa kubwa ya waislamu katika kuenzi maisha na mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). Idadi kubwa ya washiriki katika hafla hii imekuwa ishara tosha ya mafanikio makubwa ya tukio hilo takatifu, na ushahidi wa mapenzi ya kweli kwa Mtume wa Mwisho
Sala ya Jamaa ni Kinga dhidi ya Shetani. Na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) alisema: فإنَّما يأكلُ الذئبُ منَ الغنمِ القاصيةَ / “Hakika mbwa mwitu humla Kondoo aliyejitenga.”