9 Julai 2025 - 21:23
Thawabu na Faida Kuu za Kuswali Sala ya Jamaa | Madrasat Hazrat Zainab (sa) Kigamboni, Dar-es-Salam kama mfano hai katika kudumisha Sala za Jamaa

Sala ya Jamaa ni Kinga dhidi ya Shetani. Na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) alisema: فإنَّما يأكلُ الذئبُ منَ الغنمِ القاصيةَ /  “Hakika mbwa mwitu humla Kondoo aliyejitenga.”

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, Siku ya Jumatano, tarehe 13 Muharram, sawa na tarehe 9 Julai, 2025, Sala ya Jamaa ya Dhuhri na Al-Asri imesaliwa katika Madrasa ya Hazarat Zainab (sa) - Kigamboni, Dar-Es-Salam, ikiongozwa na Imam Sheikh Suleiman Isa. Kuna faida kemkem za Sala ya Jamaa (Kwa maana: Sala ya Pamoja). Kwanza kabisa ifahamike kuwa Sala ya Jamaa, ni Sala yenye thamani kubwa katika Uislamu, na imehimizwa sana na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w). Na zifuatazo ni sehemu ya thawabu na faida ya zake:

Thawabu na Faida Kuu za Kuswali Sala ya Jamaa | Madrasat Hazrat Zainab (sa) Kigamboni, Dar-es-Salam kama mfano hai katika kudumisha Sala za Jamaa

1. Thawabu Zilizoongezeka:

Mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema: “Sala ya Jamaa ni bora kuliko Swala ya mtu (kuswali) peke yake kwa daraja ishirini na saba.”

2. Kuimarisha Umoja wa Kiislamu:

Sala ya Jamaa huwakutanisha Waislamu pamoja, bila kujali tofauti za kijamii, kiuchumi au kikabila, na huimarisha undugu, mshikamano na upendo baina yao.

3. Kuonyesha Nidhamu na Utaratibu:

Sala ya Jamaa hufundisha nidhamu ya wakati, usawa mbele ya Allah (swt), na utii wa pamoja kwa Imamu — na hili ni sehemu ya mambo muhimu pia katika maisha ya kila siku ya Mwanadamu.

4. Kuimarika kwa Imani na Roho ya Ibada:

Kitendo cha Waja kuwapo pamoja na Waja wengine wa Allah (swt) katika ibada, huongeza unyenyekevu, khushuu (unyenyekevu wa moyo), na huwafanya Waumini wawe na moyo mkunjufu katika kutekeleza mambo ya wajibu wa Dini yao Tukufu.

5. Kutoa Fursa ya Mafunzo na Ukumbusho:

Sala ya Jamaa ni fursa kwa Waumini kusikia na pia kusikiliza Mawaidha, masomo ya Dini, au kuswali nyuma ya Maimamu wenye elimu na maarifa, ambao huwasilisha mafundisho ya Kiislamu baada ya Sala na kuzikumbusha nafsi zao.

6. Kinga Dhidi ya Shetani:

Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) alisema: فإنَّما يأكلُ الذئبُ منَ الغنمِ القاصيةَ /  “Hakika mbwa mwitu humla Kondoo aliyejitenga.”
Kauli hii, inamaanisha kwamba Mtu (Muumini wa Kiislamu) anayeachana na Sala Jamaa ya Waislamu huwa katika hatari ya Shetani. Shetani lazima takumuweka katika udhibiti wake.

Thawabu na Faida Kuu za Kuswali Sala ya Jamaa | Madrasat Hazrat Zainab (sa) Kigamboni, Dar-es-Salam kama mfano hai katika kudumisha Sala za Jamaa

Kutokana na umuhimu huu wa Sala ya Jamaa, na Msisitizo Mkubwa uliopo juu ya Sala ya Jamaa kutoka kwa Mtume wetu Muhammad (saww), ndio maana Madrasa hii ya Banati wa Kiislamu, ya Harzat Zainab (sa), katika moja ya mafunzo yake kwa Wasichana wa Kiislamu ni kuwasisitiza kudumu katika kuipa umuhimu mkubwa sala ya jamaa katika maisha yao ya kila siku. 

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha