10 Desemba 2025 - 00:23
Makampuni makubwa ya silaha kutoka Russia, Marekani, China na Ulaya waanza kunakili teknolojia ya Droni  "Shahed“ ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Umaarufu unaozidi kuongezeka wa drone ya Shahed ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umeleta mabadiliko makubwa katika fikra za kiulinzi duniani, na sasa mataifa yenye uwezo mkubwa yanaanza kujifunza kutoka kwa taifa lililotumia ubunifu na uhalisia badala ya gharama kubwa.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Makampuni makubwa ya kutengeneza silaha za kivita kutoka Russia, Marekani, China na Bara la Ulaya yanaelezwa kuanza kunakili au kujifunza mbinu za uundaji wa drone aina ya Shahed kutoka iran. hatua hii imechukuliwa baada ya mashirika ya kijeshi duniani kubaini kuwa teknolojia ya iran katika utengenezaji wa drone hizi ni nafuu, rahisi kutumia na ina ufanisi mkubwa katika medani za kivita.

Makampuni makubwa ya silaha kutoka Russia, Marekani, China na Ulaya waanza kunakili teknolojia ya Droni  "Shahed“ ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Drone aina ya Shahed zimejipatia umaarufu kutokana na uwezo wake wa kuruka umbali mrefu, kubeba mzigo wa milipuko, kutumia mfumo wa usambazaji wa kisasa, pamoja na gharama ndogo za uzalishaji ukilinganisha na drone za mataifa makubwa. hali hii imeifanya drone hii kuwa kivutio kikubwa kwa majeshi na makampuni ya utengenezaji wa silaha duniani.

Makampuni makubwa ya silaha kutoka Russia, Marekani, China na Ulaya waanza kunakili teknolojia ya Droni  "Shahed“ ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa baadhi ya makampuni ya Russia, Marekani, China na Ulaya yameanza kufanya tafiti za kina kuhusu teknolojia ya Droni ya Shahed, huku yakijaribu kuboresha mifano yao ili kufanana na uwezo wa drone hizo za iran. mambo yanayochunguzwa zaidi ni pamoja na:

1_Mifumo yake rahisi lakini madhubuti ya urambazaji,

2_Gharama nafuu ya vifaa vinavyotumika,

3_Muundo wake mwepesi unaoweza kurushwa kwa wingi,

4_Uwezo wa kutengeneza athari kubwa kwa bajeti ndogo.

Makampuni makubwa ya silaha kutoka Russia, Marekani, China na Ulaya waanza kunakili teknolojia ya Droni  "Shahed“ ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Wataalamu wa masuala ya ulinzi wanasema kuwa hatua hii inaonyesha jinsi teknolojia ya kijeshi ya iran ilivyofikia kiwango cha juu licha ya vikwazo vya kimataifa. inathibitisha pia kuwa katika zama hizi, si lazima nchi iwe na bajeti kubwa ili kuunda teknolojia inayoweza kubadilisha mwelekeo wa kivita.

Kwa ujumla, umaarufu unaozidi kuongezeka wa drone ya Shahed ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umeleta mabadiliko makubwa katika fikra za kiulinzi duniani, na sasa mataifa yenye uwezo mkubwa yanaanza kujifunza kutoka kwa taifa lililotumia ubunifu na uhalisia badala ya gharama kubwa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha