Hazrat Zainab (sa)
-
Somo la Qur’ani Tukufu Lafanyika Kila Wiki katika Madrasat Hazrat Zainab (s.a) Kigamboni
Programu ya kila wiki ya somo la Qur’ani Tukufu imefanyika katika Madrasat Hazrat Zainab (s.a.) Kigamboni, Dar es Salaam, chini ya ufundishaji wa Sheikh Muhammad Jaafar, kwa ushiriki wa wanafunzi wote wa madrasah hiyo.
-
Programu ya Asubuhi ya Kimaanawi Yaendelea katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni
Wanafunzi wa Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni, Dar es Salaam, wameendelea na programu ya kila siku ya asubuhi kwa kusoma Qur’ani Tukufu, dua na ziyara mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha malezi ya kiroho, maadili ya Kiislamu na uhusiano wao na Qur’ani pamoja na Ahlul-Bayt (as).
-
Ibada ya Sala ya Ijumaa Yaadhimishwa na Kuhuishwa katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni - Dar-es-Salam
Ibada ya Sala ya Ijumaa ya wiki hii ilifanyika katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni, Dar es Salaam, ikiongozwa na Hujjatul-Islam Sheikh Ghawthi Nyambwa, ambaye katika Khutba zake alizungumzia masuala muhimu ya maisha ya kila siku pamoja na matukio ya mwezi wa Rabiul-Awwal, akisisitiza maisha, haiba na nafasi ya kijamii na kisiasa ya Hazrat Zainab (sa).
-
Wanafunzi wa Madrasat Hazrat Zainab (sa) Washiriki Usomaji wa Dua ya Nudba
Asubuhi ya Ijumaa, tarehe 25 Septemba 2026, wanafunzi wa Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni, Dar es Salaam, wamehuisha ibada ya kusoma Dua ya Nudba, ikiwa ni sehemu ya utamaduni wao wa kila Ijumaa wa kuimarisha ibada, maadili na mapenzi kwa Ahlul-Bayt (as).
-
Mfululizo wa Vikao vya Qur’ani Waendelea katika Madrasat Hazrat Zainab (sa) Kigamboni, Dar es Salaam
Mfululizo wa vikao vya Qur’ani umeendelea katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni – Dar es Salaam, chini ya uongozi na ufundishaji wa Sheikh Muhammad Jaafar. Vikao hivyo vinawalenga wanafunzi wa shule hiyo na vinazingatia kukuza uelewa wa Qur’ani kupitia elimu, kuhifadhi, usomaji, tafakuri na tafsiri ya aya za Qur’ani Tukufu. Kuendeleza programu hizi kunalenga kuwajengea wanafunzi uhusiano wa karibu na Qur’ani na kuwasaidia kuelewa na kutumia mafundisho yake katika maisha yao ya kila siku.
-
Dar es Salaam: Shule ya Hazrat Zainab (s.a) Yaendesha Mafunzo ya Lugha ya Kiajemi kwa Wanafunzi wa Hawza
Mafunzo ya lugha ya Kiajemi yaandaliwa kwa wanafunzi wa Shule ya Kiislamu ya Hazrat Zainab (s.a) Kigamboni, Dar es Salaam, kwa lengo la kuwaandaa wanaotarajia kuendelea na masomo ya Hawza na elimu ya juu nchini Iran.
-
Kitabu cha “Hakimu wa Umma” chazinduliwa Kargil, India
Taasisi ya Utafiti na Elimu ya Baqir al-Ulum (as) ya Kargil, India, imeandaa mkutano wa kielimu na kifasihi wenye kaulimbiu “Sauti ya Zainab (sa)”, uliowakutanisha wanazuoni, wasomi, washairi, wanafunzi wa vyuo vya dini na vyuo vikuu. Katika hafla hiyo, kitabu “Hakimu wa Umma” kimezinduliwa, huku washindi wa mashindano ya usomaji wa vitabu kwa vijana wakitunukiwa.