Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii (Ijumaa), Tarehe 8 Agosti 2025, Dua ya Nudba imesomwa kwa muda wa dakika 30, kwa ushirikiano wa Wanafunzi wa Chuo cha Kidini cha Wasichana cha Hazrat Zainab (sa) kilichopo Kigamboni Jijini Dar-es-salaam.
Dua hii imeendeshwa na Wanafunzi wa Chuo hicho, na huo ni Utamaduni Muhimu wa Kiislamu katika kuimarisha ibada na kuongeza msukumo wa kiroho miongoni mwa washiriki kwa kuzingatia kuwa Dua ni silaha ya Waumini.
Dua ya Nudba ni moja ya dua maarufu katika Tamaduni za Kiislamu, inayoelezea shukrani, maombi ya msamaha, na kumbukumbu za Imamu Hussein (AS) na wafuasi wake.
Usomaji wa Dua wa namna hii kawaida huvutia ushiriki mkubwa wa Wanafunzi na Wapenzi wa Ibada na Dua, na kuleta hali ya utulivu wa kiibada katika mazingira ya Chuo hiki cha Kiislamu.
Your Comment