Shirika Ia Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Kikao cha kufunga mwaka cha Jamiat Al-Mustafa International Foundation kimefanyika siku ya Alhamisi, tarehe 20 Novemba 2025, katika eneo la Mbezi Beach – Makonde, Jijini Dar-es-salaam, Tanzania chini ya uongozi wa Mkuu wa Taasisi, Dkt. Ali Taqavi.

Katika kikao hiki, iliwasilishwa taarifa ya jumla kuhusu shughuli, mafanikio na changamoto za Taasisi husika katika kipindi cha mwaka uliopita. Dkt. Taqavi alisisitiza umuhimu wa:
- Kuimarisha ubora wa programu zote za Taasisi
- Kupanua huduma za kielimu na kijamii
- Kuongeza ushirikiano na taasisi za ndani na za kimataifa.

Washiriki walipata nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo ya kuboresha utendaji wa Taasisi. Mazungumzo yalikuwa ya kujenga baina ya Mkuu wa Chuo na Wanafunzi, na yalilenga kuweka mikakati madhubuti kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo unaofuata.

Mwisho wa kikao ulihitimishwa kwa msisitizo juu ya kuendelea na safari ya maendeleo kwa mpangilio thabiti, ushirikiano mkubwa na malengo yanayoeleweka.
Your Comment