Kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), mitihani yote imeendeshwa kwa utaratibu uliopangwa na kukamilika kwa mafanikio. Uongozi wa madrasa mbalimbali umeonyesha ushirikiano mkubwa, huku walimu na wasimamizi wakifanya kazi kwa uadilifu na bidii kuhakikisha kwamba kila hatua ya zoezi hili inafanikishwa kwa ufanisi.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt(as) -ABNA- Taasisi ya Hujjatul Asr Society of Tanzania, chini ya usimamizi wa Maulana Sayyid Arifu Naqvi Mwenyezi Mungu amuhifadhi, imefanikisha kwa mafanikio makubwa zoezi la mitihani ya mwisho wa mwaka 2025 kwa madrasa zote zilizo chini ya taasisi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Lengo la Mitihani
Mitihani hii imelenga kukusanya takwimu na kutathmini kiwango cha uelewa wa wanafunzi na waumini kuhusu elimu ya Uislamu, ikizingatia mafundisho sahihi ya Ahlul Bayt (a.s). Zoezi hili limekuwa chachu ya kuboresha mitaala, mbinu za ufundishaji, na kuongeza ubora wa elimu katika madrasa zote zinazoratibiwa na taasisi.

Utekelezaji wa Zoezi
Kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), mitihani yote imeendeshwa kwa utaratibu uliopangwa na kukamilika kwa mafanikio. Uongozi wa madrasa mbalimbali umeonyesha ushirikiano mkubwa, huku walimu na wasimamizi wakifanya kazi kwa uadilifu na bidii kuhakikisha kwamba kila hatua ya zoezi hili inafanikishwa kwa ufanisi.

Shukurani na Dua
Taasisi inamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukamilisha jukumu hili muhimu. Shukurani za dhati pia zinatolewa kwa watumishi wote wa Hujjatul Asr Society kwa kujitolea kwao katika kufikisha ujumbe wa Ahlul Bayt (a.s). Aidha, tunawashukuru wale wote wanaotoa juhudi zao za hali na mali kwa ajili ya kuendeleza harakati za tabligh chini ya mwavuli wa taasisi.

Tunaomba Mwenyezi Mungu awazidishie taufiki, afya na uwezo katika kuendelea kulitumikia Dini Tukufu ya Uislamu.

Your Comment