Jamii
-
Falsafa ya Maombolezo na Kumbukumbu ya A'shura | Kulinda Haki na Uhuru wa Watu ni Muhimu zaidi kuliko Maisha binafsi
Haki ya mtu binafsi na umma: Imam Hussein alijua kwamba alikuwa akielekea kifo, lakini alikusudia kuonyesha ulimwengu kuwa kulinda haki na uhuru wa watu ni muhimu kuliko maisha binafsi. Maombolezo ya Ashura yanatufundisha kuwa watu wanapaswa kuwa tayari kujitolea, si tu kwa ajili ya nafsi zao, bali kwa ajili ya ustawi wa jamii.
-
Mwakilishi wa Palestina katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa: "Fanikisha kuwasukuma Waisraeli kusitisha mauaji ya kimbari yanayoendelea"
Mwakilishi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amemshitaki utawala wa Kizayuni wa Israel kwa ukiukaji wa sheria za kimataifa na hukumu za Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICC), na kuhimiza hatua madhubuti kutoka kwa nchi za dunia ili kuzuia uhalifu unaoendelea wa utawala huo katika Ukanda wa Gaza. Ametoa msisitizo kuwa mashambulizi yanayofanywa mara kwa mara na Israel dhidi ya raia wasio na hatia na kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia, ni hali inayotakiwa kupokelewa kwa uzito mkubwa na jamii ya kimataifa.
-
Safari ya Kuleta Umoja ya Ayatollah Ramezani nchini Niger; Mazungumzo na Maulamaa Wakuu wa Dini wa Mji wa Niamey | Zawadi ya Pete ya Baraka Yatolewa
Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) katika kikao na Imam wa Msikiti Mkuu wa Mji wa Niamey alisisitiza umuhimu wa kuimarisha Umoja wa Kiislamu na kuunga mkono nafasi ya Wanazuoni wa Dini katika jamii.
-
"Ayatollah Ramezani: Dini inapaswa kuwa na ufanisi katika nyanja mbalimbali za kitamaduni, kisiasa na kiuchumi"
"Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) alisema: Tunapaswa kuwa na mtazamo jumuishi kuhusu dini ili tuone athari kamili za dini; mtazamo jumuishi maana yake ni kwamba dini ina sura ya nje na ya ndani, ina wajibu wa mtu binafsi na pia wajibu wa kijamii. Haiwezekani dini iwe na hukumu nyingi za kijamii lakini isiwe na Serikali."
-
Sheikh Dkt. Abdul- Razak Amiri Atoa Kisa Halisi Cha Mwanamke wa Kiislamu aliyedai Talaka kisa Mume Wake Kaoa Mke wa 2, Hatimaye naye akawa Mke wa Pili
Ndoa ni heshima, ndoa ni stara ya kijamii, na ndio maana Qur'an Tukufu ikasema: «هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ» kwamba "Mwanamke ni vazi kwa Mwanaume, na Mwanaume ni vazi kwa Mwanamke". Katika kazi za vazi (nguo) ni heshima, kupendeza, kuheshimika, vazi kawaida yake linaleta heshima katika jamii, na Ndoa vile vile inaleta heshima katika Jamii.
-
Hatua Tano na Muhimu Kabla ya Kuingia Katika Mjadala au Kabla ya Kufanya Mjadala na Mtu yeyote | Bila hatua hizi huo sio Mjadala Bali ni Kupoteza Muda
Kabla hujafanya mjadala wowote na mtu yeyote, unapaswa kuzingatia nukta za kimjadala na muhimu ili uepuke mapema kupoteza muda wako kwa kuingia katika mjadala usiokuwa na matunda yoyote.
-
Nukta 7 na Muhimu za Tabia Njema, Zilizosheheni Hekima na Busara
"Mwenyezi Mungu ameumba Viumbe Tofauti tofauti, na kila kimoja amekipa sifa zake , Ni Tatizo sana unapo taka Sifa za Kuku awenazo Bata".
-
Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi nchini Iraq katika mazungumzo na Abna:
Kuhifadhi Utukufu wa Ramadhani na kuimarisha matumaini, ni sababu ya Nguvu na Ukaribu wa Kiislamu
Ayatollah Hosseini, Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Iraq na mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi ameashiria taathira za funga kiutamaduni na kijamii na kusisitiza juu ya ulazima wa kuhifadhi utukufu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika jamii.