Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, utafiti mpya wa maoni nchini Marekani unaonyesha kuwa msaada wa Wamarekani kwa utawala wa Israel umepungua.
Katika utafiti uliofanywa na gazeti la New York Times, ripoti inaonyesha:
-
1- 40% ya Wamarekani wanasema Israel inaua kwa makusudi raia (Wapalestina), ikilinganishwa na 20% tu baada ya shambulio la Oktoba 7.
-
2- Wengi wa wapiga kura wa Marekani wanapingana na kuongezwa kwa misaada ya kifedha na kijeshi kwa Israel.
-
3- 35% ya Wamarekani sasa wanapendelea Palestina, ikilinganishwa na 20% baada ya Oktoba 7.
-
4- Msaada wa Wamarekani kwa Israel umepungua hadi 34%, ikilinganishwa na 47% baada ya shambulio la Oktoba 7.
Your Comment